Mkurugenzi wa Idara
ya Maendeleo ya Jamii Bw. Patrick Golwike akizungumza na washiriki wa mkutano
wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya
Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati)
aweze kufungua mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa
Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Mkuu wa Chuo
cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni Mwenyekiti wa mafunzo (kulia) Bw.
Paschal Mahinyika akiwatambulisha washiriki wa mafunzo ya kudhibiti viashiria
hatarishi kabla ya kukaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga (katikati) aweze kufungua mafunzo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo
31.7.2017.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga
(katikati) akizungumza na Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa
ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo
yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani
Morogoro leo 31.7.2017.
Washiriki wa mafunzo ya udhibiti wa
viashiria hatarishi kutoka vyuo vya Maendeleo ya Jamii vinavyosimsmiwa na
Wizara wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Katibu Mkuu (hayupo pichani)
wakati wa uendeshaji wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo 31.7.2017.
Watendaji kutoka Wizara ya Afya, Mendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto(Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii) kutoka kulia ni
Mkurugenzi Utawala na Rasilimali Watu Utawala na Rasilimali watu Bibi Deodata
Makani , katikati ni Mkurugenzi wa Ugavi na Manunuzi Bibi Martha chuma na
kushoto ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani Bibi Lightness Mchome wakimsikiliza Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba
Nkinga(hayupo pichani) katika ufunguzi
wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani Morogoro leo
31.7.2017.
Mkurugenzi
Utawala na Rasilimali Watu Utawala na Rasilimali watu kwa kutoka Wizara ya Afya,
Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Deodata Makani akitoa somo juu
ya masuala ya kuzingatia kwa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii wakati wa
ufunguzi wa Mafunzo ya Udhibiti wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji wa Vyuo hivyo
yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti, mkoani
Morogoro leo 31.7.2017.
Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi Sihaba Nkinga(kushoto)
akijadiliana jambo na Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare ambaye ni
mwenyekiti wa mafunzo Bw. Paschal Mahinyika(kulia) wakati wa mafunzo ya ya Udhibiti
wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo vya maendeleo ya Jamii
yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani
Morogoro leo 31.7.2017.
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto akiwasilisha mada
kuhusu uaandaaji mzuri wa Bajeti kwa Wakuu wa Vyuo vua Maendeleo ya
Jamii nchini katika mafunzo ya ya Udhibiti
wa Viashiria Hatarishi katika Utendaji kwa wakuu wa Vyuo hao
yanayofanyika katika Ukumbi wa Wakala wa Mbegu za miti , mkoani
Morogoro leo 31.7.2017.
Picha
na Erasto Ching’oro WAMJW
...............
Na
Erasto Ching’oro WAMJW
Katibu
Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo
ya Jamii) Bibi. Sihaba Nkinga amewahimiza Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii,
kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utendaji wao wa kazi katika
kuendesha vyuo wanavyovisimamia.
Ameyasema
hayo wakati akifungua mafunzo kwa wakuu wa vyuo hao kuhusu udhibiti wa viashiria hatarishi vya
utendaji na utawala ikiwa ni pamoja na kuzingatia
nidhamu ya matumizi ya fedha katika utendaji wao wakazi wa kila siku ili kuepuka
hoja za ukaguzi wa fedha.
Amesisitiza
kuwa wakuu wa vyuo ni watumishi wa Umma na wanapaswa kuzingatia weledi mahala
pa kazi kwa mujibu wa sheria kanuni na taratibu zote za utumishi wa Umma katika
kutimiza majukumu yao.
“Niwatake
Wakuu wa Vyuo mliopo hapa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo katika
kundesha vyuo mnavyoviongoza tuondokane na dosari katika suala la udhibiti wa Fedha
katika matumizi” alisema Bibi Sihaba.
Aidha,
Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga, amesema kuwa mara baada ya mafunzo haya maalum, Vyuo vya
Maendeleo ya Jamii nchini vitaweza kufuta hoja zote za ukaguzi mahala pa kazi
kutokana na kufanya kazi kwa kufuata maadili, maarifa na miongozo na weledi unaotakiwa
katika uendeshaji wa vyuo.
Aidha Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amewataka wakuu wa vyuo kuongeza umakini katika utekelezaji wa majukumu
yao mahala pa kazi, kuimarisha mawasiliano katika uwajibikaji wa pamoja kwa
kuimarisha mifumo ya utendaji kazi katika vyuo vya maendeleo ya jamii.
Mafunzo
haya yameandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee na Watoto (Idara
Kuu Maendeleo ya Jamii) na kushirikisha vyuo vya Buhare, Uyole, Rungemba, Ruaha,
Mabughai, Monduli na Mlale.










0 Comments