Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiwapungia mkono wananchi wakati akitembelea mabanda mbalimbali baada ya
kufungua rasmi maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa katika viwanja
vya Mwalimu Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam leo. Rais
Magufuli ameyafungua rasmi Maonyesho hayo, yaliyoanza Juni 28 - Julai
8, 2017, ambapo kwa ushauri wake, Maonyesho haya kwa mwaka huu
yameongezewa siku tano zaidi na kutarajiwa kumalizika Julai 13, 2017.
Picha na Ikulu.





0 Comments