- Mkuu wa mkoa wa Mbeya leo amezindua mkakati wa kukuza utalii Mkoa wa Mbeya
- Ameutangaza Mkoa wa Mbeya kuwa ni LANGO la UCHUMI na UTALII nyanda za Juu kusini
- Amesema mkakati huo wa kukuza utalii ni muhimu kwasababu Mkoa wa mbeya na mikoa YA nyanda za juu kusini ina vivutio vingi na vizuri lakini havijatangazwa ikiwemo hifadhi ya Ruaha , Kitulo , ziwa Ngozi, Daraja la Mungu, maporomoko ya Maji na Fukwe za ziwa Nyasa
- Sekta YA utalii ni YA pili kwa kuchangia pato la Taifa hivyo ni muhimu kuendekezwa
- Kwa kuwa na uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa songwe,Barabara KUU ya kuunganisha Mkoa wa Mbeya na nchi za Kusini na Uwepo wa meli Tatu mpya ziwa Nyasa Mkoa wa Mbeya ni Lango la uchumi kwani kutaongeza biashara na uwekezaji
- Anesema Mkoa wa Mbeya ni Mkoa wa Tatu kwa Kuchangia Pato la Taifa BAADA YA Dsm na Mwanza
- Amewaomba wananchi, taasisi mbalimbali kutangaza utalii na kuwahamasisha wawekezaji kuwekeza ktk mahoteli na usafirishaji kukuza utalii




0 Comments