Serikali
kupitia Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imesema imeandaa mtaala mpya
ambao umeandaliwa katika misingi ya elimu jumuishi ambao ulianza kutumika kuanzia
mwaka wa masomo 2014/2015 ili kumudu wanafunzi wenye mahitaji maalum.
Hayo yamesemwa
na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Eng,Stella Manyanya wakati
akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe.Stella Ikupa Alex aliyetaka kujua
Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kila mwalimu anapatiwa mafunzo maalum
yatakayomwezesha kufundisha wanafunzi wenye ulemavu.
“Hadi sasa
wahitimu wa ngazi ya Stashahada ya Elimu maalum wapatao 158 wamehitimu Octoba
2016 na wanachuo 248 wanaendelea na masomo katika chuo cha Ualimu Patandi”,Aliongeza
Mhe.Manyanya.
Aidha Waziri
uyo amesema kuwa kutokana na umuhimu wa walimu hawa Wizara yake katika mwaka wa
fedha 2016/17 iliendesha Mafunzo kwa walimu 519 walio kazini wanaofundisha darasa la kwanza na la pili
kuhusiana na mtaala ulioboreshwa ili kumudu ufundishaji wa wanafunzi wenye
mahitaji maalum.
Pamoja na hayo
tarehe 20 mpaka 28 Juni,2017 walimu 712 walio kazini wanaofundisha wanafunzi
wenye ulemavu wa akili na wenye usonjo walipatiwa mafunzo katika vituo vya
Mwanza,Arusha,Mbeya na Morogoro ili kuwajengea uwezo wa kumudu ufundishaji wa
wanafunzi wenye ulemavu huo.
“Walimu 600
wanaofundisha darasa la tatu na nne watapatiwa mafunzo ya Mtaala ulioboreshwa
kuanzia tarehe 10 hadi 30 Julai,2017 lengo ni kuwafikia wengi zaidi”Alisisitiza
Mhe.Manyanya.

0 Comments