Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo akizungumza na
wananchi wa Rorya na kuwapongeza kwa ujenzi wa madarasa na mabweni.
Mbunge wa Vitimaalum Agnes Marwa akizungumza na wananchi wakati wa ziara ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo akikata utepe na
kuweka jiwe la msingi katika shule ya sekondari Nyamtinga wilayani
Rorya.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Selemani Jafo
amewapongeza viongozi na watendaji wa wilaya na halmashauri ya wilaya ya
Rorya kwa mahusiano mazuri waliyonayo katika kuwaletea wananchi
maendeleo.
Jafo alitoa sifa hizo alipokuwa wilayani humo kwa ziara ya kikazi ya kukagua miradi na kuongea na watumishi
Katika
ziara hiyo, Jafo alifanikiwa kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa,
mabweni, maabara, na vyoo kwa sekondari ya Nyamtinga na Nyamunga ambapo
majengo hayo yamebainika kujengwa kwa ubora wa kuridhisha.
Ujenzi wa miundombinu hiyo imegharimu zaidi ya sh.milioni 500 kutoka serikali kuu kwa lengo la kuboresha elimu hapa nchini
Kwa
upande wake,Mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara, Agness Marwa
amempongeza Naibu Waziri huyo kwa kufika wilayani Rorya na kwamba
amekuwa Waziri pekee aliyefanikiwa kutembelea wilayani humo katika
kipindi hiki cha serikali ya awamu ya tano.
Mbunge huyo ameishukuru serikali kwa upendo wake wa kuisaidia wilaya hiyo miradi ya maendeleo.
Naibu
Waziri Jafo leo amekamilisha ziara yake ya kikazi ya siku sita ya
kukagua miradi ya maendeleo na kuongea na watumishi kwa mkoa wa Kagera
na Mara na anaendelea na ziara yake katika mikoa mingine.




0 Comments