Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wakazi wa Mbeya baada ya
kuwasili kwenye Viwanja vya Ruanda Nzove jijini humo kuhutubia mkutano
wa hadhara, Julai 31, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos
Makalla.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea kiwanda cha vinywaji baridi
cha SBS- Pepsi kilichopo eneo la Iyunga jijini Mbeya, Julai 31, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na watoto wa Shule Wenye
Ulemavu ya Child Support Tanzania ya jijini Mbeya baada ya kuwasili
kwenye kiwanda cha vinywaji baridi cha SBS- Pepsi kilichopo Iyunga
jijini Mbeya Julai 31, 2017.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Methadone Clinic ambao ni maalum
kwa kuwahudumia na kuwapa ushauri nasaha waathirika wa madawa ya kulevya
kwenye . hospitali ya Rufaa ya Mbeya Julai 31, 2017. Kushoto ni Mbunge
wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Salim Jessa
(wanne kushoto) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu
kilichopo Iyunga jijini Mbeya wakati alipoembelea kiwanda hichi Julai
31, 2017. Watatu kushoto ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson
Mwansasu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Salim Jessa
(kulia) ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Malumalu
kilichopo Iyunga jijini Mbeya wakati alipoembelea kiwanda hicho Julai
31, 2017. Kushoto kwake ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson
Mwansasu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye
Viwanja vya Ruanda Nzove jijini Mbeya Julai 31, 2017.
(Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)








0 Comments