Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto anayeshughulikia Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii
Bibi
Sihaba Nkinga(kushoto) akisalimiana na mjumbe wa Kamati Kuu ya Baraza la
Watoto Taifa Lulu Nziku mara baada ya kumaliza mkutano na Baraza la
kata ya mseke iringa Vijijini hivi karibuni.
Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW.
.............................................
Na Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini, WAMJW.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia wazee na
watoto (Idara Kuu ya Maendeleo ya jamii) Bibi Sihaba amewataka Maafisa Ustawi
wa Jamii katika halmashauri zote nchini kutekeleza wajibu wa uundaji wa Kamati
za Ulinzi na Usalama wa mtoto kuanzia ngazi ya mtaa mahali walipo wananchi ili
kuwa na mfumo thabiti wa kuzuia na kutoa huduma kwa watoto wanaofanyiwa
ukatili.
Ameyasema hayo mapema wiki hii wakati wa kikao cha majumuhisho
kwenye kilele cha safari yake ya kikazi katika kijiji cha Tanangozi, kata ya
Mseke, tarafa ya Mlolo, wilaaya ya Iringa vijijini mkoani Iringa na kupokea
taarifa za utetezi wa haki za watoto kutoka kwa Baraza la Watoto la Kata ya
Mseke, Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mtoto, na Timu ya malezi ya watoto wa Kata
ya Mseke.
Ameongeza kuwa mabaraza ya watoto yakianzishwa na kuimarishwa
katika ngazi za vijiji na kata yatasaidia kutoa raghiba ya watoto kujitambua,
kujithamini na kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili na pia kujiepusha na vishawishi
vya mahusiano na wanaume katika umri mdogo.
Aidha, Katibu Mkuu aliwapongeza wajumbe wa vyombo hivyo
vilivyoundwa na watoto na wazazi kuendeleza wajibu wao wa kuzuia na kutokomeza
ukatili na nyanyasaji wa watoto katika
ngazi ya familia, jamii na shuleni ili kuongeza ubora wa jamii zetu katika
utoaji wa haki za msingi za watoto wote katika jamii zetu.
Alisema Serikali imekamilisha mwongozo wa utekelezaji wa Mpango
Kazi wa Taifa wa kutokomeza dhidi ya wanawake na watoto hapanchioni amabo
utasambazwa kwa wadau ili kutoa maelekezo fasaha ya utendaji katika maeneo ya
utekelezaji wa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Katibu Mkuu Bibi Sihaba Nkinga amesisitiza kutumia vikundi vya malezi ya watoto na sanaa
katika Kata ya Msewe, Wilaya ya Iringa Vijijini kwa kujiunga pamoja na kutumia
stadi na mbinu walizonazo katika kuelimu jamii kuacha vitendo vya ukatili dhidi
ya watoto ili kuimarisha mazingira upatikanaji wa haki na usawa kwa wototo
wote.

0 Comments