Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ( kushoto) akieleza jambo wakati wa kikao na
Maafisa Utamaduni na watendaji wa Mkoa
wa Pwani katika ziara yake ya kikazi jana mkoani hapo lengo ikiwa ni kuwahamasisha maafisa hao
kufanya kazi kwa kuzingatia utamaduni wa
kutunza na kuheshimu muda ili kuleta matokeo chanya kwa jamii kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Bibi. Joyce Fisoo.
Baadhi ya wajumbe wa kikao waliohudhuria kikao
kazi wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel Jana Mkoani Pwani.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa kwanza kushoto) akimsikiliza Mkuu wa
kituo cha Makumbusho cha Caravan Serai Bibi.
Reinfrida Kapela (kulia) wakati wa ziara
yake ya kikazi jana Mjini Bagamoyo,
katikati ni Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo Bibi. Erica Yegela.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel ( kulia) akipata maelekezo kutoka kwa Mkuu wa kituo cha Makumbusho cha Caravan
Serai Bibi. Reinfrida Kapela (kushoto)
namna ambavyo wanawake wa Mji wa Bagamoyo walivyokuwa na utamaduni wa kutengeneza
urembo wa liwa kwa kutumia jiwe wakati
wa ziara yake ya kikazi jana Mjini hapo.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo
kwa Mkuu wa kituo cha Mji Mkongwe Bw.
Noel Laswai (katikati) katika ziara yake
ya kikazi Wilayani Bagamoyo kulia ni Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo Bibi.Erica
Yegela
(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM)






0 Comments