Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Uthibiti wa
Ubora wa Mbolea Tanzania (TFRA) Lazaro Kitandu akisisitiza jambo wakati wa
mkutano wake na Waandisi wa Habari kuhusu mfumo mpya wa uagizaji wa mbole kwa
pamoja leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Issa Sabuni.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Uthibiti wa
Ubora wa Mbolea Tanzania (TFRA) Lazaro Kitandu akionyesha orodha ya bei elekezi
kwa mbolea za DAP ya kupandia na UREA ya kukuzia mazao wakati wa mkutano wake
na Waandisi wa Habari kuhusu mfumo mpya wa uagizaji wa mbole kwa pamoja leo
Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Issa
Sabuni.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Uthibiti wa
Ubora wa Mbolea Tanzania (TFRA) Lazaro Kitandu (katika) akisisitiza jambo
wakati wa mkutano wake na Waandisi wa Habari kuhusu mfumo mpya wa uagizaji wa
mbole kwa pamoja leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Issa Sabuni na kushoto ni Mkaguzi wa Mbolea
kutoka TFRA, Allan Mariki.
Baadhi ya waandishi
wa habari wakifuatilia mkutano wao na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa
Ubora wa Mbolea Tanzania (TFRA) Bw. Lazaro Kitandu (hayupo pichani) leo Jijini
Dar es Salaam.
Picha na: Idara ya
Habari - MAELEZO
...........................
Na.
Paschal Dotto-MAELEZO
Wakulima wanatarajia
kupata mbolea kwa bei nafuu tofauti na hapo zamani ambapo hivi sasa Serikali
imekuja na mfumo mpya wa uagizaji wa mbolea kwa wakulima wote katika maeneo
yote Tanzania hususani maeneo ya vijijini ambako mbolea ilikuwa inafika kwa
gharama kubwa.
Akizungumuza Jijini
Dar es Salaam leo Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Udhibiti wa Ubora wa Mbolea
Tanzania(TFRA) Bw. Lazaro Kitandu amesema kuwa huduma ya upatikanaji wa mbolea
kwa wakulima wote nchini utarahisishwa kwa kuwa Serikali kupitia Wizara ya Kilimo
na Mifugo imeweka utaratibu mpya wa uagizaji wa mbolea kwa kutoa tenda kwa
wazabuni mbalimbali.
“Serikali imechukua
hatua ya kuanzisha utaratbu mpya wa kuagiza mbolea kwa pamoja kutoka
zinakotengenezwa, yaani mbolea za kupandia (DAP) na mbolea za
kukuzia(UREA) kupitia kwa wawekezaji
wanaochukua zabuni hiyo”,alisema Kitandu.
Hatua nyingine ambazo
serikali imechukua katika kuboresha sekta ya kilimo ni pamoja na Mamlaka hiyo
kuweka matarajio ya matumizi makubwa ya mbolea ili kuendana na kasi ya nchi za Kusini
mwa Jangwa la Sahara.
Tanzania ina matumizi
ya asilimia 19 ya mbolea kwa hekta moja ambayo ni matumizi madogo,nchi nyingine
zina matumizi ya asilimia 50 kwa hekta moja kwa hiyo mamlaka inaweka matarajio
makubwa kwa matumizi ya mbolea ili kuinua kilimo na kujenga uchumi wa viwanda.
Aidha Bw. Kitandu
alisema mchakato wa kumpata mzabuni wa kazi hiyo ya uagizaji mbolea ulianza
mwezi Aprili kwa kutangaza zabuni kwa makampuni mbalimbali ambapo kufikia mwezi
Julai, 2017 washindi walipatikana ambao ni kampuni ya OCP ya Morocco na Premium
Agrocam ya Tanzania.
“kufuatia utaratibu
huu mpya mchakato ulianza tangu mwezi aprili kwa kuchuja watu ambao wanauwezo wa kutuleta mbolea ,lakini
mchakato uliendelea mwezi Julai tukapata mzabuni wa mbolea za kupandia(DAP)
ambapo Kampuni ya OCP kutoka Morocco ilibuka washindi katika zabuni hiyo na
kumpuni ya Premium Agrocam kuwa mzabuni wa mbolea ya kukuzia yaani (UREA)”,
alisema Bw. Kitandu.
Bw.Kitandu alivitaja
vigezo vilivyotumika kumpata mzabuni huyo kuwa ni pamoja na bei inayopatikana
katika viwanda vinavyotengeneza mbolea ambapo OCP pamoja na premium agrocam walionekana
kuwa na bei za kuridhisha.
Aidha Bw. Kitandu aliwahakikishia wakulima kuwa mbolea itasafirishwa mpaka vijijini kwa kutumia
treni na malori kwa sehemu ambapo treni haiwezi kufika, na amewatoa hofu wakulima kuwa msimu unaoanza
mwezi wa tisa wameagiza tani 23,000 kwa mbolea ya kupandia (DAP) na tani 32,000
kwa mbolea ya kukuzia (UREA) ambapo watakuwa wanaagiza kwa awamu kwa miezi
miwili miwili.
Tanzania inatumia Tani
4000,000 kwa mwaka na kwa kwa msimu huu bei ya mbolea itashuka kutoka aslimia
15 mpaka asilimia 40, ambapo kwa mfuko wa kilo 50 utanunuliwa kwa shilingi
.52,000 badala ya shilingi 1000,000 bei ya awali.
Pia amewaonya wale
watakaotumia mwanya huu kuuza mbolea nje ya bei elekezi ya Serikali kwamba
watachukuliwa hatua za kisheria kama kunyang’anywa leseni, kufungwa, faini au
vyote kwa pamoja.




0 Comments