Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wajumbe wa Bodi ya ya
Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) baada ya kupokea Ripoti ya
Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma ambapo
ameahidi kuzichukulia hatua taasisi zote zilizokiuka taratibu za manunuzi
zilizoainishwa kwenye Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha
2016/2017.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya
Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga (kushoto) akiongea wakati
wakimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya Tathmini
ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, Kulia ni Mjumbe wa Bodi hiyo Prof. Sufian
Bukurura.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi
ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern
Lumbanga wakati wa makabidhiano ya Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa
Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya
Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga akimkabidhi Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha
2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akionesha kwa wanahabari na wajumbe
wengine wa Bodi(hawapo pichani) kitabu cha Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa
Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, , Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi
ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern
Lumbanga.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akikata utembe baada ya kupokea Ripoti
ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, Kulia ni
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya
Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga.
Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi
ya Umma (PPRA) Dkt. Laurent
Shirima akiongea, wakati wakimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip
Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini
Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.
Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya ya Mamlaka ya
Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA).
PICHA NA IDARA YA
HABARI-MAELEZO
....
Na:
Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Serikali imesema
itazichukulia hatua Taasisi zote zilizokiuka sheria na kanuni za manunuzi ya
Umma pamoja na zile zenye viashiria vya rushwa ambazo zimebainika katika ripoti
ya tathmini ya utendaji iliyotolewa na Mamlaka
ya Udhibiti wa Manunuzi
ya Umma (PPRA) kwa
mwaka wa Fedha 2016/17.
Hayo yamesemwa leo
Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango alipokuwa akipokea ripoti ya tathimini ya utendaji wa Taasisi za Serikali katika sekta ya
Manunuzi iliyofanywa na PPRA kwa mwaka wa Fedha 2016/17.
“Tutazichukulia hatua
na kuziwajibisha taasisi zote ambazo zimebainika katika ripoti hii kuwa na
viashiria vya rushwa au kufanya malipo
yenye utata katika manunuzi yao,” alisema Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango amesema
kuwa, zaidi ya 70% ya fedha za Umma zinatumika kununua vifaa na huduma
mbalimbali hivyo Serikali haitavumilia kuona fedha hizo zinatumika bila kufuata
sheria na kanuni zilizowekwa.
Aidha, Mwenyekiti wa
Bodi ya Wakurugenzi wa PPRA Balozi Dkt. Matern Lumbanga amezitaja taasisi
ambazo zimekiuka sheria na taratibu za manunuzi kwa mwaka 2016/2017 kuwa ni
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Taasisi ya Mifupa (MOI) pamoja na Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taasisi nyingine ni
Shirika la Bima la Taifa (NIC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Mamlaka ya Anga
(TCAA), Wizara ya Fedha na Mipango na Halmashauri ya Wilaya Kondoa.
Balozi Lumbanga
amesema kuwa uchunguzi wa zabuni mbili zenye thamani ya shilingi bilioni 160.5
ambazo zilikuwa zinatekelezwa na Wizara ya Fedha na Mipango pamoja TCAA
haukubainika mapungufu ya msingi na PPRA ilipendekeza utekelezaji wa miradi
hiyo uendelee kama ilivyopangwa.
“Uchunguzi uliofanywa
katika taasisi sita zilizobaki ulibaini kuwa Serikali ilipata hasara ya
takribani shilingi milioni 12.15 kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo,
ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi uliosababisha ongezeko la riba pamoja
na faini zilizotokana na ukiukwaji wa taratibu za kijamii na mazingira kabla ya
kuanza kwa utekelezaji wa kazi za ujenzi,” alisema Balozi Lumbanga.
Balozi Lumbanga
amezitaja Taasisi zilizobainika na malipo yenye utata kuwa ni Mfuko wa Taifa wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF), Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na Halmashauri ya
Kwimba. Ukaguzi wa kupima upatikanaji wa thamani ya fedha ulibaini malipo yenye
utata katika taasisi hizo tatu ambazo ni kiasi cha shilingi milioni 483.44
zililipwa kwa wakandarasi kwa kazi ambazo hazikuwa zimefanyika.
Vile vile amesema
kuwa, miradi 33 katika taasisi 17 ilibainika kuwa na kiwango kikubwa cha
viashiria vya rushwa. Taasisi hizo ni Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka za
Moshi (Muwasa), Mwanza (Mwauwasa) na Arusha (Auwasa) pamoja na Halmashauri ya
Wilaya za Wilaya za Msalala, Kibondo na Moshi.
Taasisi byingine ni
Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Wizara ya Maji na
Umwagiliaji, Chuo cha Ufundi Arusha, Halmashauri ya Mjia wa Kahama, Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Uhasibu Arusha (IAA), Ofisi ya Katibu Tawala
Mkoa wa Kilimanjaro, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Halmashauri ya Mji wa MAsasi pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha
Arusha (AICC).
Ripoti hiyo ni ripoti
ya 11 kuwasilishwa Wizara ya Fedha na Mipango tangu PPRA ilipoanzishwa.










0 Comments