Wasanii
wa kikundi cha Kakau Band kutoka Bukoba wakitumbuiza katika jukwaa la Tanzania
wakati wa mchana.
Wasanii wa kikundi cha Taifa cha Utamaduni cha Wizara ya Habari Utamaduni
Utalii na Michezo Zanzibar wakicheza ngoma ya Msewe ambayo ni maafuru Kisiwani
Pemba.
Watanzania
wakishangilia na kucheza katika JAMAFEST aliyevaa safari suti ni
Naibu Balozi wa Tanzania nchini Uganda Bw.
Elibariki Maleko.
Wasanii
wa kikundi cha Taifa cha Wizara Habari,
Utamaduni, Utalii na
Michezo Zanzibar wakicheza ngoma ya asali
ya Zanzibar.
Aliyesimama
na kushika Microphon Bw. Iddi Suwed Mkurugenzi Mkuu wa
Kikundi cha taifa cha tarabu cha Wizara ya Habari,
Utamaduni, Utalii na
Michezo Zanzibar wakati wakitumbuiza nchini
Uganda.
Aliyevaa suti ya bluu na skafu ya bendendera ya Jamuhuri
ya Muungano wa Tanania ni Kaimu Balozi ambaye
pia ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Bw. Elibariki Maleko, aliyevaa
shati jeupe ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa
Tanzania Bara Profesa Elisante Ole Gabriel wa Naibu Katibu Mkuu wake Bi. Nuru
Milao wakiangalia ngoma za utamaduni katika unoesho la usiku.
Baadhi ya Watanzania wakiangalia ngoma za
utamaduni wakati wa onesho la sanaa usiku.
...
Tamasha la Sanaa na Tamaduni la
Jumuiya ya Afrika Mashariki JAMAFEST limeanza rasmi jana katikati ya mji wa
Kampala kwa wasanii wa sanaa za ubunifu za
ngoma za utamaduni kwa kuoneshwa bidhaa zao mbali mbali za Nchi
Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Katika jukwaa la Tanzania Kikundi
cha Taifa cha Utamaduni cha Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo cha
Zanzibar, Jinogile Band, Kakau Band na
kikundi cha Taarabu cha Taifa cha Zanzibar vilitia fora na kuwa kivutio kikubwa
kwa wananchi waliofika katika Tamasha hilo.
Tamasha
la Utamaduni na Sanaa la Jumuiya ya Afrika Mashariki linatarajiwa kufunguliwa
rami leo na Rais wa Uganda Kaguta Yoweri Museveni katika viwanja vya Kololo na
kauli mbiu ya Tanasha hili ni Utamaduni na ubunifu wa viwanda ni injini ya
umoja na ajira
JAMAFEST ni tamasha lenye lengo la
kuwaunganisha wasanii wasanaa za ubunifu za utamaduni kwa kutafuta soko la
bidhaa hiyo adimu yenye wazalishaji wengi katika nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki ambayo inakuza sekta ya utalii
katika Jumuiya na kwa mwaka huu Tanzania imewakilishwa na washiriki zaidi ya
200.
Washiriki wa Tanzania katika
maonesho ya jana kwa upande wa Tanzania yaliongozwa na Kaimu Balozi ambaye pia
ni Naibu Balozi wa Tanzania Nchini Uganda Bw. Elibariki Maleko, Mshauri wa Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi wa Mambo ya Utamaduni na
Utalii Mhe. Chimbeni Kheri, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii
na Michezo wa Tanzania Bara Profesa Elisante Ole Gabriel wa Naibu Katibu Mkuu wake
Bi. Nuru Milao pamoja na Watanzana wanaoishi na kusoma nchini Uganda.
Washiriki wa Tanzania wamekuwa na
lengo la kuonesha bidhaa ngoma za
utamaduni, nguo, shanga, dawa za mitishamba, lugha ya kiswahili, vyakula,
mapishi na ulimbwende.
Habari
na Picha
Wizara ya Mambo y Nje n Ushirikiano
wa Afrika Mashariki









0 Comments