Picha na Maktaba.
......
Na:
Mwandishi Wetu
Makundi mawili kila
moja likiwa na wastani wa wakimbizi 350 raia wa Burundi kati ya wakimbizi
13,000 ambao hadi tarehe 07 Septemba, 2017 walikuwa wamejiorodhesha kwa hiari
kurejea nyumbani yanatarajiwa kuondoka nchini wiki hii.
Kwa mujibu wa
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Wakimbizi, katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Deusdedit Masusu, misafara saba yenye wastani wa wakimbizi 350 inatarajiwa
kuondoka nchini kurejea Burundi katika mwezi huu wa Septemba, 2017 miwili kati
ya hiyo ikiondoka siku ya Jumanne tarehe 12 na Alhamisi tarehe 14 Septemba,
2017.
Bwana Masusu
aliieleza Idara ya Habari- MAELEZO ofisini kwake hivi karibuni kuwa idadi ya
wakimbizi wataorejeshwa nyumbani inatarajiwa kuongezeka kadri zoezi hilo ambalo
lilianza Alhamisi wiki iliyopita litakavyoshika kasi.
“Mpango wetu
unaonesha kuwa kwa mwezi huu wa Septemba wakimbizi waliondoka tarehe 7 na
wengine wataondoka tarehe 12, 14, 19, 21, 26 na 28 kwa watani wa wakimbizi 350”alisema
lakini hata hivyo alieleza kuwa kundi la kwanza lililoondoka lilikuwa na
wakimbizi 301 tu.
Mkurugenzi Msaidizi huyo
alieleza kuwa kasi ya kujiandikisha kwa hiari kwa wakimbizi hao raia wa Burundi
inatarajiwa kuongezeka zaidi kufuatia makundi hayo kurejea nyumbani kwa kuwa
mafanikio ya zoezi hilo yatakuwa kichocheo kwa wengine kutaka kurejea nyumbani.
“Tunatarajia ikifika
mwishoni mwa mwezi huu kasi ya kujiorodhesha itaongezeka sana kwa kuwa
watakaorejea watatoa taarifa zaidi kwa wenzao hivyo kwa wale wanaosita bila ya
shaka wengi wao hawataona sababu ya kuendelea kubaki makambini” Alisema bwana
Masusu.
Alibanisha kuwa
urahisi wa mawasiliano utawezesha wakimnizi waliorejea kuwapa wenzao mrejesho
wa hali ilivyo nchini kwao na hivyo kutoa hamasa kwa walioko makambini nao
kutaka kurejea nyumbani.
Mkurugenzi Msaidizi huyo
aliongeza kuwa kinachofanyika ni kuhakikisha zoezi hilo linafanyika kwa umakini
mkubwa na kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa ili wakimbizi hao waweze kurejea
nyumbani kwa usalama na heshima.
“Shirika la Kimataifa
la Uhamiaji (IOM) ndilo linalotoa usafiri wa wakimbizi na mzigo yao kutoka
makambini hadi nchini Burundi na wakimbizi wanaorejea wanasaidiwa chakula
kupitia Shirika la Mapngo wa Chakula (WFP) kwa miezi mitatu” Alifafanua bwana Masusu.
Zoezi la kuwarejesha
wakimbizi hao wa Burundi linafanyika kufuatia makubaliano yaliyofikiwa tarehe
31 Agosti, 2017 jijini Dar Es Salaam kati ya Serikali za Tanzania, Burundi na
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR).
Zoezi la kuwarejesha
wakimbizi kundi la kwanza, kwa upande wa Tanzania, lilishuhudiwa na Mkuu wa
Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali (Mstaafu ) Emmanual Maganga, Kamati ya Ulinzi
na Usalama wa Mkoa Kogoma pamoja
Mwakilishi wa UNHCR nchini na maafisa wengine wa Wizara ya Mambo ya Ndani.
Msafara wa Burundi
uliongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Nchi hiyo Theranse Ndayiragije,
Mwakilishi kutoka Ofisi ya UNHCR Burundi na washiriki wengine. Tukio hilo
lilishuhudiwa pia na Ofisa Ubalozi wa Tanzania nchini Burundi.

0 Comments