Meneja Chapa na Masoko
Airtel Tanzania Anorld Mandale akishika bango baada ya kuzindua huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambapo wateja wataweza kufaidi
huduma hii kwa kupiga *150*60# na kujipatia 1GB, dakika150 kwa muda wa
siku saba. Kushoto ni Meneja Ubora
wa huduma za Mtandao wa Airtel Tanzania Emmanuel Luanda na Meneja Uhusiano
Airtel Tanzania Jackson Mmbando
Meneja
Uhusiano wa AIRTEL Tanzania Jackson Mmbando akizungumza na waandishi wa habari
leo katika uzinduzi wa programu mpya ya
Airtel U900 ambao lengo lake kuu ni kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa
huduma bora kwa wateja wake mahali popote nchini. Mradi Tayari ushazinduliwa na
kuwasha mitambo kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha. Kulia ni
Meneja Ubora wa huduma za Mtandao Emmanuel Luanda
Meneja Ubora wa huduma za
Mtandao wa Airtel Tanzania Emmanuel Luanda akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam baada ya kuzindua programu mpya ya Airtel U900 ambao lengo
lake kuu ni kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake
mahali popote nchini. Kushoto ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Jackson
Mmbando. Teknolojia hii itaongeza upatikanaji wa
mtandano wa 3G kwa Asilimia 50 zaidi pamoja na kuongeza ubora wa upatikaniji wa
intaneti bila kujali maeneo mteja alipo.
Meneja Chapa na Masoko
Airtel Tanzania Anorld Mandale baada ya kuzindua programu mpya ya Airtel U900 ambao lengo lake kuu ni
kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote
nchini. Kampuni hiyo pia huduma ya Bando la OFA KABAMBE
ambapo wateja wataweza kufaidi huduma hii kwa kupiga *150*60# na
kujipatia 1GB, dakika150 kwa muda wa siku saba.
............
• Teknolojia ya U900 kuwapatia watumiaji wa Airtel Intaneti yenye kasi popote.
•Airtel yawekeza kwenye teknolojia mpya ya intaneti kutoa mtandao bora hata ukiwa ndani ya jengo.
Airtel Tanzania Plc kampuni
ya mawasiliano iliyojikita katika huduma zenye ubunifu wa teknolojia
zaidi nchini, leo katika muendelezo wake wa kutimiza dhamira yake ya kuwa
mtandao bora zaidi imetangaza na kuzindua rasmi programu yake ya maboresho ya
huduma za mtandao wake kupitia teknolojia ya iliyopewa jina la ‘Mradi wa
U900’ ukiwa na lengo la
kuimarisha ubora wa mtandao na kutoa huduma bora kwa wateja wake mahali popote
nchini.
Mradi wa U900 ni uwekezaji mkubwa unaolenga
kuhakikisha uhakika wa upatikanaji wa huduma ya 3G, ujazo wa data kamili pamoja
na kuongeza kasi ya intaneti kwa kutumia teknolojia hii ya mawimbi ya
mawasiliano ya masafa ya 900 Mhz. Teknolojia hii itaongeza upatikanaji wa
mtandano wa 3G kwa Asilimia 50 zaidi pamoja kuongeza ubora wa upatikani wa
intaneti bila kujali maeneo mteja alipo, Popote utapata Intaneti bora.
Akiongea leo jijini Dar es Salaam wakati wa
kutangaza huduma hiyo, Meneja Ubora
wa huduma za Mtandao Airtel, Emanuel Luanda alisema
kuwa Airtel imewekeza kwenye kuimarisha huduma ya mtandao kutokana na ongezeko
la matumizi ya simu za smartphone na pia kutokana na uhitaji wa huduma mpya za
ziada. Kutokana na uboreshaji wa mtandao wetu, wateja wote nchini watakuwa
wakitapa huduma yenye kasi na hivyo kuwa na uhakika na huduma bora kutoka
Airtel wakiwa popote.
Bw, Luanda alidokeza “ripoti ya hivi karibuni
ya TCRA inayotoa mchanganuo wa matumizi ya huduma za Intaneti (Data)
inaweka wazi kuweko kwa ongezeko la watumiaji wa huduma za intaneti kutokea 34%
kwa mwaka 2015 na kupaa hadi 40% kwa mwaka 2016. Hali hiyo ndio inatoa
msukumo hata kwetu Airtel kuendelea kuwekeza zaidi katika teknolojia mpya
ili kuwapatia wateja wetu huduma bora zaidi”.
“Tayari tushafanya maboresho kwenye miji ya
Dar es Salaam, Arusha na Mwanza huku maboresho mengine yakiendelea kufanyika
Dodoma, Morogoro na miji mingene yenye uhataji mkubwa wa huduma zetu hapa
Tanzania.” Alieleza Luanda
Kwa upande wake, Meneja wa Masoko Airtel Tanzania Arnold Madale
alisema, “kwa kuwa Airtel tunatambua mahitaji ya wateja wetu, hali ya soko
tumekuwa tukifanikiwa kuleta bidhaa zenye ubunifu na mpangilio wa huduma
zinazozingatia mahitaji ya mteja, hii ni hatua kubwa sana hasa kwenye ushindani
wa biashara. Tunao wateja ambao wanatumia mtandao wetu kwa ajili ya intaneti
tu, lakini pia kuna wale wanaotumia kwa kupiga na kupokea simu, tunazo bidhaa
na huduma ambazo zinakidhi matakwa ya wateja hao kwa muda wote wakiwa mahali
popote.
Kwa sasa hivi tunaendelea pia kuboresha huduma yetu ya 2G ili kutoa
huduma yenye uhakika wa hali ya juu ikiwemo huduma ya Airtel Money ili
kuendelea kuwafikia Watanzania wengi waishio pembezoni huduma za kibenki
na huku tukitimiza sera ya serikali ya kushiriki katika uboreshaji wa huduma
bora za kifedha vijijini.”
“Tunapotangaza huduma hii muhimu ya kuboresha
mtandao wetu, tunayo furaha kutangazia huduma ya Bando la OFA KABAMBE ambayo
inapatika kwa urahisi na kumfanya mteja kuwa na Uhuru zaidi wa kutumia Intaneti
yenye kasi kwa muda mrefu zaidi kwa kuwasiliana na ndugu, marafiki
au wadau katika biashara mahali popote. Wateja wetu wataweza kufaidi
huduma hii ya bando kwa kupiga *150*60# na kujipatia 1GB, dakika150
kupiga mitandao yote na kudumu nazo kwa muda wa siku saba, aliongeza Madale.
‘Nia yetu ni kuendelea kukua kupita Maelezo
huku tukitengeneza ujuzi wa kuaminiwa na wateja wetu kwa kuwa na gharama nafuu.
Mradi wa U900 unadhihirisha kuwa Airtel imeamua kuinua taifa letu kufikia lengo
la kuishi kidigitali kwa kuwepo na huduma za kidigitali, aliongeza Madale.





0 Comments