Pichani ni Bw. Jeremiah Ragita aliyejifanya kuwa
Wakili akitokea Kampuni ya Sheria ya Faithful Attorney Advocates kwa
mujibu wa Naibu Msajili, Mahakama ya Ardhi, Mhe. Frank Mahimbali anasema
Wakili huyo feki alikamatwa mapema Novemba 08 katika Mahakama hiyo akimsimamia
Mleta maombi Nunu Mhusin Mkwata.
.....
Mhe. Mahimbali anasema kuwa upande wa pili ambao
unasimamiwa na Wakili Maros Gabriel kutoka Kampuni ya Sheria ya 'Common Law
Chambers' ulimtilia shaka Bw. Jeremiah Ragita kama kweli ni Wakili ndipo
alipofanya upekuzi kwenye Ofisi ya TLS na kuambiwa kuwa hawana jina hilo.
Hata hivyo Mhe. Mahimbali alienda mbali na
kumuandikia barua Msajili wa Mahakama Kuu (RHC) na kujibiwa kuwa hakuna Wakili
aliyesajiliwa kwa jina hilo.
Kwa mujibu wa Naibu Msajili kesi hiyo ilipoitwa
mbele ya Mhe. Jaji Crencesia Makuru, Wakili Maros alimueleza Mhe. Jaji kuwa
mwenzake wa upande wa pili sio Wakili na kisha akatoa vielelezo kutoka katika
Ofisi ya Msajili Mahakama Kuu na Ofisi ya TLS ndipo Bw. Ragita akakiri kuwa
yeye si Wakili.
Hata hivyo Bw. Ragita alikamatwa na kupelekwa
Polisi Kituo cha Kati (Central Police) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya hatua
stahiki za kisheria.
Mahakama inapinga vikali vitendo vya ulaghai
(Mawakili feki, vishoka) vinavyofanywa na baadhi ya Wananchi kwa lengo la
kujipatia kipato.
(Imetolewa na Kitengo cha Habari, Elimu na
Mawasiliano, Mahakama)

0 Comments