Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza kikao cha
Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichofanyika katika
Ukumbi wa White House mjini Dodoma. Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa
CCM Zanzibar Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, Katibu Mkuu wa CCM
Abdulrahman Kinana pamoja na Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula.
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman
Kinana akizungumza katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) kilichofanyika katika Ukumbi wa White House mjini Dodoma.
Wajumbe
wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiimba mara baada ya
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli kuwasili
katika ukumbi wa Chama cha Mapinduzi (White House) mjini Dodoma.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Waziri Mkuu Mstaafu
Dkt. Salim Ahmed Salim akiwaaga wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi
(CC) mara baada ya kumaliza muda wake.
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye amemaliza muda wake Waziri Mkuu
Mstaafu Dkt. Salim Ahmed Salim.
Picha na IKULU







0 Comments