Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akikagua Dawa katika stoo ya Dawa
katika Kituo cha Afya Mazwi, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mkoa wa
Rukwa wilaya ya Sumbawanga, pembeni yake ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt Boniface
Kasululu.
![]() |
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akijiridhisha na uwepo wa Dawa katika
stoo ya Dawa katika kituo cha Afya cha Mazwi.
|
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiteta jambo na viongozi mbali mbali
katika moja ya jengo jipya linalojengwa katika kuboresha kituo cha Afya cha
Mazwi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Dkt. Faustine ndugulile akiongoza msafara wa ukaguzi wa jingo
jipya katika kituo cha Mazwi Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa.
Na WAMJWW. RUKWA-SUMBAWANGA
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Rukwa kuhakikisha
wanapambana na kutokomeza udumavu kwa watoto unaosababishwa na ukosefu wa Lishe
bora.
Ameyasema hayo akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya
kukagua shughuli za utoaji huduma za Afya, na uhamasishaji wa vikundi vidogo
vidogo vya wanaweke vya ujasiriamali
katika Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
Mkoa wa Rukwa haupaswi kuwa na utapiamlo hata kidogo,
asilimia 60 ya udumavu ndani ya Rukwa ni kiasi kikubwa sana, katika mkoa ambao
una chakula na ardhi yenye rutuba nzuri ni jambo la kushangaza kuona tatizo
hili?, Alisema Dkt. Ndugulile
Dkt. Ndugulile aliendelea kwa kusema kuwa, Siku 100 za
mwanzo tangia mtoto anazaliwa ni muhimu na nyeti sana katika kuhakikisha anapata maziwa ndani ya miezi sita, na
anapoanza kula ale vyakula vyenye lishe ya kutosha ili ubongo wake ukue vizuri.
Aidha, Dkt. Ndugulile ametoa maelekezo kwa sekretarieti ya
Mkoa na viongozi wa kisiasa kushirikiana kwa pamoja katika kutoa elimu ya
kutosha kwenye kila mikusanyiko watakayofanya kuhusiana na masuala ya Lishe
bora ili kutokomeza janga hili linalosumbua idadi kubwa ya watoto katika Mkoa
huu.
Kwa upande wake Mbunge wa Sumbawanga Mh. Aishi Hilaly
amemshukuru Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Faustine Ndugulile kwa kuwakumbuka
katika mgao wa fedha za kuboresha Vituo vya Afya cha Mazwi, pia hakusita kupaza
sauti juu ya ombi la gari la kubebea wagonjwa litakalosaidia kupunguza hadha
kubwa wanayokumbana nayo inayotokana na kukosekana kwa gari hilo.
Nae Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Boniface Kasululu Mkoa
unaendelea kupambana na magonjwa ya mlipuko hasa ugonjwa wa kipindupindu kwa
kutoa elimu ya Afya na Usafi wa mazingira kwa wananchi, ili kuhakikisha
magonjwa haya yanakuwa historia katika mkoa wa Rukwa.
Aidha, Dkt. Kasululu alimuomba Dkt. Faustine kupunguza hadha
ya upungufu wa madaktari bingwa na mabingwa wa fani nyingine, Dkt. Kasululu
alisema kuwa hadi kufikia Desemba 2017 Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa
inajumla ya madaktari bingwa 5 ambao ni sawa na asilimia 21 kati ya madaktari
24 wanaohitajika






0 Comments