Random Posts

Man utd yamtengea dau Neymar

Imeripotiwa kuwa Manchester United wameamua kutoa dau la £444m kwa ajili ya nyota wa Paris Saint-Germain Neymar.

Wakati wa majira ya joto, Neymar alihama kwa dau la rekodi ya dunia kutoka Barcelona kwenda Parc des Princes, na Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili amefunga magoli 20 katika mechi 22 za michuano yote.
Hata hivyo hofu imezuka kuhusu furaha ya mchezaji huyo mwenye miaka 25 katika Ufaransa na Real Madrid inaaminika kuwa tayari kutoa dau nono kumsajili mchezaji huyo ikiwa atakuwa sokoni miezi 18 ijayo.
Miamba wa La Liga hata hivyo wanaweza kukabiliwa na ushindani kutoka kwa United, kwani miamba hao wa Uingereza wanajiandaa kutoa dau la £444m kwa ajili ya mchezaji huyo, kwa mujibu wa Le 10 Sport.
Ofa hiyo itaipita kwa mbali £365m ambayo inaaminika Madrid walitaka kutoa kwa ajili ya nyota huyo, kwani United watakuwa na wepesi wa kuzungumza.
Mkataba wa Neymar na vinara hao wa Ligue 1 unafika kikomo 2022.http://sokaglobe.co.tz

Post a Comment

0 Comments