Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pilia kulia)
akisalimiana na viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania TAWA, muda mfupi baada ya kuwasili makao makuu ya
mamlaka hiyo mkoani Morogoro jana.
.............................. .....................
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameugiza uongozi wa
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kukabidhi eneo la Kilomita za
mraba 25,000 kutoka kwenye Hifadhi ya Msitu wa Morogoro unaosimamiwa na
wakala huyo kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za Makao Makuu ya Mamlaka ya
Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).
Ametoa
agizo hilo jana akiwa kwenye ziara ya siku mbili mkoani Morogoro ambapo
alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mej. Jen. Gaudence Milanzi
kuzikutanisha taasisi hizo ndani ya siku saba zijazo ili kukamilisha
mchakato wa kumega eneo hilo na kukabidhiwa kwa Mamlaka hiyo ili
taratibu za ujenzi ziweze kuanza.
Aidha,
ameuagiza uongozi huo wa TFS kuweka vigingi vya mpaka katika eneo la
hifadhi hiyo ya msitu ndani ya siku 30 zijazo huku akitoa muda huo huo
kwa wananchi wote waliovamia eneo hilo kuondoka mara moja kwa hiari yao
wenyewe kabla ya kuondolewa kwa nguvu.
Katika
hatua nyingine, Dk. Kigwangalla amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala
hiyo, Prof. Dos Santos Silayo kukabidhi mbao zaidi ya 400 zilizokamatwa
hivi karibuni mkoani Morogoro baada kuvunwa kinyume cha Sheria kwa
uongozi wa Mkoa huo ili zisaidie kutengeneza madawati ya shule za
msingi.
Pamoja
na mbao hizo amemuagiza pia mtendaji huyo kukabidhi kwa uongozi wa mkoa
huo magunia 350 ya mkaa yaliyokamatwa katika kituo cha Tazara yakiwa
yanasafirishwa kinyume cha Sheria ili yasambazwe kwenye shule za
Sekondari mkoani humo.
Dk.
Kigwangalla alitoa maagizo hayo jana wakati akizungumza na Kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo,
Dk. Steven Kebwe, ambapo alimuomba kusimamia zoezi hilo la ugawaji
kikamilifu ili walengwa waweze kufikiwa.
Katika ziara hiyo ametembelea pia bonde la Kilombero ambalo ni chanzo kikubwa cha maji yanayotengeneza Stieglers Gorge ambapo Serikali ya awamu ya tano itajenga mradi mkubwa wa kuzalisha umeme wa megawatts 2100. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa pilia kulia) akisalimiana na viongozi na watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA, muda mfupi baada ya kuwasili makao makuu ya mamlaka hiyo mkoani Morogoro jana. Dk. Kigwangalla akizungumza na watumishi wa TAWA wakati wa ziara hiyo.u

0 Comments