Waziri ummy Mwalimu akiangalia ramani ya kituo hicho cha afya
ambacho kimejengwa kwa ushirikiano wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema
na Shirika la SEDA Foundation, kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Dkt.Subi na kushoto ni mmoja wa Viongozi wa Shirika hilo.
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia Ramani ya Ujenzi wa jengo la
ghorofa nne la Uzazi linalojengwa hospitali ya Mkoa ya Sekoture jijini
Mwanza.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto akiangalia kazi inavyoendelea katika hospitali hiyo
Waziri Ummy Mwalimu na Naibu Waziri Dkt.Angela Mabula wakikagua
ujenzi wa jengo la dharura la uzazi kwenye kituo cha afya cha Karume
kilichopo kata ya Igombe Wialayani Ilemela,akiyevaa koti la bluu ni
Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt.Florian Tinuga
Waziri Ummy Mwalimu akiangalia duka la dawa lililopo kwenye
hospitali ya Mkoa ya Sekoture ambapo upatikanani wa dawa kwa Mkoa wa
Mwanza ni asilimia 80.
Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy
Mwalimu akikagua huduma za afya kwenye kituo cha afya cha kamanga
kilichopo Wilaya ya Sengerema.Waziri ummy yupo Mkoani Mwanza katika
ziara ya kikazi ya kujionea hali ya utoaji huduma za afya mkoani hapo.
Jengo la Maabara lililojengwa kwenye kituo hicho cha afya katika
mpango wa Serikali wa kuboresha huduma za dharura za uzazi kwenye vituo
vya afya nchini.
(Picha zote na Wizara ya Afya)







0 Comments