Mshauri elekezi wa mradi wa upanuzi na ujenzi katika Chuo Cha
Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc Arch.
Benjamini Kasiga aliyevaa fulana ya bluu akiwakilisha mada katika kikao
kifupi kilichofanyika chuoni hapo wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo
hiko uliofanywa na jopo la Wakaguzi kutoka Wizara ya Afya Mkoani Mtwara.
Mkandarasi kutoka kampuni ya Ujenzi na Uhandisiz Nandhra wa
kwanza kushoto akiwapa maelezo baadi ya wakaguzi wa jengo hilo kutoka
Wizara ya Afya wakati wa ukaguzi wa majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara
na Chuo Cha Maafisa Tabibu Mtwara CoTc uliofanyika leo mkoani humo.
Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha kusanifu Majengo Wizara ya Afya
Arch. Daniel Mwakasungura aliyevaa shati jekundu akiangalia moja ya
sehemu ya jengo la Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC na Chuo Cha Maafisa
Tabibu Mtwara CoTc wakati wa ukaguzi wa majengo ya chuo hiko uliofanyika
leo mkoani humo, katikati ni Mratibu wa ujenzi huo Dkt. Joachim
Catherine na kulia ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi Wizara
ya Afya Bw. Castro Simba.
Jengo la wagonjwa Kutoka nje la
Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambalo lipo kwenye ujenzi bado
ambapo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1. 7 za Kitanzania na
lengo la ujenzi wa Hospitali hiyoni kuweza kutoa huduma za kibingwa.
Picha Na Wizara ya Afya-MTWARA
Baadhi ya Majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara NTC Chuo Cha Maafisa
Tabibu Mtwara na CoTc yakiwa yamekamilika katika mradi wa ujenzi wa
Ujenzi,Upanuzi na ukarabati wa majengo ya chuo hiko na Chuo Cha maafisa
Tabibu mtwara yalipokaguliwa na wakaguzi wa jengo hilo kutoka Wizara ya
Afya leo mkoani Humo.
NA WAMJW-MTWARA
SERIKALI Kupitia Wizara ya Afya imeagiza Kampuni ya Ujenzi na
Uhandisi Nadhra kumalizia kazi ya kurekebisha kasoro zilizotokana na
ujenzi katika majengo ya Chuo Cha Uuguzi Mtwara ( NTC) na Chuo cha
Maafisa Tabibu mkoani humo (COTC) ili kuweza kudahili wanafunzi wengi
zaidi.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Ununuzi na Ugavi Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bw. Castro Simba
wakati wa ukaguzi wa majengo hayo mkoani Mtwara.
“Majengo haya yalimalizika Desemba 2016 tukatoa kipindi cha
mwaka mmoja kujiridhisha na ubora wake lakini kuna baadhi ya maeneo
hayajakidhi ubora hivyo mkandarasi anatakiwa kurekebisha ndani ya mwezi
mmoja” alisema Bw. Simba.
Aidha Bw. Simba amesema kuwa mradi huo wa kupanua, kukarabati
na kujenga majengo hayo yanafanyika katika vyuo vitano nchini ikiwemo
Hospitali ya Kairuki Dar es salaam, Bagamoyo, Chuo cha Uuguzi Mtwara
(NTC), Chuo Cha Maafisa Tabibu (CoTC) na Chuo cha St. Bakhita cha
Sumbawanga.
Kwa upande wake Mratibu wa Kuimarisha Mifumo ya Afya na
Mratibu wa Mradi huo kutoka Wizara ya Afya Dkt. Joachim Catherine
amesema kuwa mradi huo uliofadhiliwa na Global Fund umehusisha ujenzi
Wa mabweni matatu yenye vyumba 120, Nyumba za watumishi nane katika chuo
cha maafisa tabibu. Katika na Chuo cha uuguzi Mtwara.
Aidha Dkt. Catherine amesema kuwa Miradi yote imegharimu
kiasi cha Shilingi bilioni 3.3 za kitanzania na kulifanyika ukarabati
na upanuzi Wa madarasa, ofisi za wakufunzi, maktaba pamoja na maabara za
vitendo.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Uuguzi Mtwara (NTC) Bw.
Frolian Mbungu amesema kuwa amefurahishwa na ukaguzi huo kwani utamfanya
apokee majengo kwa kujiamini na kuyatumia kwa ufasaha.
Aidha wakaguzi hao kutoka Wizara ya Afya wakiongozwa na
Mkurugenzi wa Sera na Mipango Dkt. Edward Mbanga walitembelea jengo la
wagonjwa Kutoka nje la Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kusini ambalo
limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 1. 7 za Kitanzania na lengo la
ujenzi wa Hospitali hiyo ni kuweza kutoa huduma za kibingwa.







0 Comments