Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzina Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (wa kwanza kushoto) akimhoji Mhandisi Magesa Mwita wa TANROADS, Mbeya kuhusu taarifa anayoitoa kwake ya maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la abiria la uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya wakati wa ziara yake uwanjani hapo
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzina Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la abiria la uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya wakati wa ziara yake uwanjani hapo
Muonekano wa jengo
jipya la abiria ambalo halijamalizika ujenzi wake la uwanja wa ndege wa Songwe,
Mbeya kama lilivyokutwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani)
wakati wa ziara yake uwanjani hapo
Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzina Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye (katikati) akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la abiria la uwanja wa ndege wa Songwe, Mbeya wakati wa ziara yake uwanjani hapo
Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi
Atashasta Nditiye (wa pili kushoto) akipita kwenye eneo la uwanja wa ndege wa
Mbeya ambao wananchi wamepimiwa viwanja 75 vya makazi kimakosa ambapo Serikali
inaurejesha kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, mmiliki halali wa eneo
hilo ili uendelezwe. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Bwana William
Paul Ntinika
Naibu Waziri wa
Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.
Mhandisi Atashasta Nditiye ameielekeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania
(TAA) kumfikisha mahakamani mkandarasi anayejenga jengo jipya la abiria la
uwanja wa ndege wa Songwe lenye uwezo wa kuchukua abiria 1,500,000 kwa mwaka.
Mhandisi Nditiye
ametoa maelekezo hayo kwa TAA wakati wa ziara yake uwanjani hapo ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la abiria la uwanja huo. “Naielekeza TAA
kuchukua hatua za kisheria kwa kampuni hii ya DB Shapriya na kumpeleka
mahakamani mkandarasi huyu kwa kuwa mkataba wa miezi minane umechukua miaka
mitano na Serikali imeshamlipa fedha zote tangu mwaka 2015”, amefafanua
Mhandisi Nditiye.
Amesisitiza kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli haiko tayari kumvumilia
mkandarasi yeyote anayetumia vibaya pesa ya Serikali ya wananchi walipa kodi,
hivyo mkandarasi huyu ataitema fedha hii.
Mhandisi Nditiye
ameongeza kuwa Serikali itamshitaki mkandarasi huyu kwenye Bodi ya Usajili wa
Wakandarasi na Serikali haiko tayari kuendelea kufanya kazi na wakandarasi wa
namna hii. Aidha, amewahakikishia wananchi watanzania kuwa jengo hilo
litakamilika na Serikali itatafuta mkandarasi mwingine.
Mhandisi Nditiye
ameitaka TAA kuanzia tarehe 31 Januari mwaka huu ambapo ilipewa maelekezo na
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ianze kuikata fidia
ya uchelewashaji wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo mkandarasi huyo.
Naye Mhandisi Mshauri
wa kampuni ya kiuhandisi ya UNETEC kutoka Dubai Mhandisi Silanda Dustan amesema
kuwa mkandarasi hajafikia kiwango kinachotakiwa cha kujenga jengo hilo la
abiria ambapo wananchi wanakosa huduma na Serikali inakosa mapato.
Serikali iliingia
mkataba wa kazi ya kujenga jengo jipya la abiria la uwanja huo na mkandarasi DB
Shapriya wa Tanzania wa gharama ya shilingi bilioni kumi na moja. Mkataba huo
ulisainiwa mwezi Februari mwaka 2013 na kazi ya kujenga jengo hilo jipya la
abiria ilitarajiwa kukamilika ndani ya miezi minane hadi mwezi Oktoba mwaka
2013.
Akiwa uwanjani hapo, Mhandisi
Nditiye ametembelea uwanja huo ili kukagua na kujiridhisha kuhusu suala la
ukosefu wa taa za kuongoza ndege ambapo jambo hilo limezungumzwa kwenye vikao
baina ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Kamati ya Bunge ya Kudumu
ya Miundombinu. Amebaini kuwa uwanja huo hauna taa na hauwezi kufanya kazi saa 24
ambapo lengo la Serikali ni kuufanya uwanja huo kuwa wa kimataifa na kwa sasa
unahudumia abiria wa nchi za jirani za Malawi, Zambia na RDC Congo.
Meneja wa Uwanja wa
ndege wa Songwe, Mbeya Bwana Hamisi Amiri amesema kuwa tayari mkandarasi wa
kampuni ya GECI Ispanola amepatikana kwa ajili ya kuweka taa za kuongoza ndege
kwa gharama ya shilingi bilioni 4.7 ambapo inajumuisha taa za barabara ya
kuruka na kutua ndege na taa za barabara. Ameongeza kuwa uwanja wa ndege wa
Songwe una uwezo sawa na uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere wa Dar es
Salaam wa kutua ndege kubwa ambapo kiwanja kina ukubwa wa eneo la hekari 1,800
na barabara ya kutua na kuruka ndege yenye urefu wa mita 3333 na upana wa mita
45.
Katika hatua nyingine
Mhandisi Nditiye ametembelea uwanja wa ndege wa Mbeya wenye ukubwa wa hekari
179 uliovamiwa na wananchi ambapo maafisa ardhi wasio waaminifu wamepima
viwanja 75 vya makazi na kuwapatia wananchi, na amelaani kitendo hicho na
Serikali itawachukulia hatua maafisa waliohusika.
Pia amewaelekeza TAA kuwekeza
kwenye uwanja huo kwa kushirikiana na sekta binafsi kwa kuwa Serikali imefuta
hati za viwanja hivyo na itaipatia TAA hati miliki ya eneo lake. Pia,
amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Amos Makalla kwa kufuatilia eneo hilo na
kuzuia wananchi kuliendeleza.
Naye Katibu Tawala
Msaidizi wa Miundombinu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Jeremia Minja amefafanua kuwa
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bwana Amosi Makalla amesimamisha zoezi la wananchi
kumiliki viwanja vya makazi na ameielekeza TAA kujipanga kuendeleza eneo hilo.
Meneja wa uwanja wa
ndege wa Songwe, Mbeya Bwana Hamisi Amiri amesema kuwa TAA itapima eneo hilo
haraka mara baada ya kupata hati miliki kutoka kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
0 Comments