Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala
ya Ukimwi na Madawa ya kulevya, Mhe. Matter Salum akiongoza uchaguzi wa
kumchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo katika kikao kilichofanyika
jana katika kumbi za Bunge Mjini Dodoma.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki,
Maadili na Madaraka ya Bunge wakifuatilia uchaguzi wa kumteua Mwenyekiti na
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo uliofanyika jana katika kumbi za Bunge Mjini
Dodoma.
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki,
Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. Eng. Ramo Makani akiongoza uchaguzi wa
kumchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo katika kikao kilichofanyika
jana katika kumbi za Bunge Mjini Dodoma.
Mwenyekiti
wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, Mhe. Jasson
Rweikiza (katikati) akizungumza na Wajumbe wa kamati hiyo baada ya kuteuliwa
kuendelea tena na nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika jana katika kumbi za
Bunge Mjini Dodoma. Wa nne kulia waliokaa, ni Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo,
Mhe. Mwanne Mchemba
(PICHA
NA OFISI YA BUNGE)
0 Comments