Balozi wa Kuwait
nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem, akizungumzia uhusiano mzuri ambao
umeendelea kuwepo kati ya Tanzania na Kuwait alipomtembelea Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)(hayupo pichani), ofisini kwake Mjini
Dodoma.
Maafisa Waandamizi
wa Wizara ya Fedha na Mipango na Ubalozi
wa Kuwait wakifuatilia kwa umakini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hawapo pichani) kuhusu
ujenzi wa barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma, katika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na
Mipango Mjini Dodoma.
Kamishna wa Fedha
za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga (Kulia) na Afisa
mwandamizi kutoka Ubalozi wa Kuwait wakifuatilia mazungumzo ya Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Balozi wa Kuwait nchini
Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) kuhusu ufadhili wa ujenzi wa barabara za
Mkato za kuingia Makao Makuu ya Nchi Mjini Dodoma.
Msaidizi wa Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt.
Philip Isdor Mpango (Mb), Bw. Edwin Makamba na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Hangi Laban, wakifuatilia mazungumzo
kati ya Waziri huyo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem
(hawapo pichani), Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akizungumza jambo na
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga
(katikati) baada ya kuagana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem
(hayupo pichani) alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Balozi wa Kuwait
nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akimkabidhi zawadi Waziri wa Fedha
na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea kwa
mazungumzo Mjini Dodoma.
Balozi wa Kuwait
nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akiagana na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip
Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na
Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akizungumza jambo na
Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga
(katikati) baada ya kuagana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem
(hayupo pichani) alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.
(Picha
na Kitengo cha Mawasiliano Selikarini Wizara ya Fedha na Mipango)
Benny
Mwaipaja, WFM, Dodoma
Dodoma,
Machi 23, 2018: Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa
Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), imeahidi kuipatia Tanzania
mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 207.3, sawa na shilingi bilioni 466.4, kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko
wa kuingia katikati ya mji wa Dodoma pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara kutoka
Morogoro hadi Dodoma, yenye urefu wa kilometa 257.
Ahadi
hiyo imetolewa mjini Dodoma na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Jassem Ibrahim
Al-Najem, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Mpango.
Balozi
Al-Najem amesema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na
kutoka mjini Dodoma zitasaidia kuondoa msongamano wa magari yanayopita katikati
ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya
Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma.
Aliahidi
kuwa nchi yake kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait na taasisi washirika (Mifuko
ya Waarabu) wa mfuko huo, wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa
ufadhili wa ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu na kilimo ili
iweze kukuza uchumi na maisha ya watu wake.
Katika
kipindi cha miaka 40, Serikali ya Kuwait, kupitia Kuwait Fund, imeipatia
Tanzania mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni
608 kwa ajili ya kutekeleza miradi 14 ya kiuchumi katika sekta za barabara,
kilimo, umeme, Maji na Afya.
Baadhi
ya miradi hiyo ambayo imekamilika ni pamoja na barabara ya Dar es Salaam hadi
Somanga inayohusisha pia ujenzi wa Daraja la Mkapa, Kiwanda cha Karatasi
Mufindi, Mradi wa kuzalisha Umeme unaotokana na nguvu ya maji-Mtera, na gharama
za upembuzi yakinifu wa upanuzi wa Bandari ya Zanzibar.
Kwa
upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru
Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake wa Maendeleo wa Kuwait kwa kuisaidia nchi
kutimiza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia mikopo yenye
gharama nafuu inayotolewa na taasisi hiyo.
Dkt.
Mpango alisema kuwa mwaka jana, Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait uliipatia Tanzania
mkopo nafuu wa shiingi bilioni 115
kwa ajili ya kuboresha barabara ya Chaya hadi Nyahua (km 85) kwa kiwango cha
lami pamoja na mradi wa maji safi na salama wa miji ya Same na Mwanga mkoani
Kilimanjaro na sehemu ya eneo la wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wenye thamani
ya shilingi bilioni 77,
Mradi
mwingine ni ufadhili wa ukarabati wa hospitali ya Mnazi Mmoja-Zanzibar
utakaogharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 13.6 sawa na shilingi bilioni 31.
0 Comments