Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Machi 18, 2018 ameanza ziara ya siku
tatu Pemba ikiwa na lengo la kuhamasisha shughuli za maendeleo.
Makamu wa Rais ambaye amewasili Pemba
alasiri ya leo na kupokelewa na viongozi mbali mbali wa Serikali na Chama
ambapo alipokea taarifa za mikoa miwili ya Pemba.
Pia Makamu wa Rais alizuru kaburi la Dkt.
Omar Ali Juma lililopo Wawi, Pemba na kuweka shada la maua.
Aidha Makamu wa Rais aliwataka Wananchi wa
Chumbageni kukumbuka historia na kurudi nyumbani, Makamu wa Rais aliyasema hayo
mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Tawi la CCM Chumbageni Wambaa.
Kesho Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan anatazamiwa kuendelea na ziara yake ambapo ataweka jiwe la msingi katika
Kituo cha Huduma za Mama na Mtoto Shumba Vyamboni .

0 Comments