Random Posts

Miradi Mikubwa ya maji bagamoyo na ruvu juu kutatua kero ya maji

 Mkuu wa Mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo ,(anaeonyesha Kidole)akielekeza jambo wakati alipotembelea baadhi ya miradi ya maji ikiwemo ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhia maji wilayani Bagamoyo,ambapo aliambatana na uongozi wa mamlaka ya maji na usafi na maji taka Dar es salaam (DAWASA).(picha na Mwamvua Mwinyi)
Mkuu wa Mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo wakati alipotembelea baadhi ya miradi ukiwemo ule wa kupeleka maji kwenye eneo la uwekezaji na ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhia maji wilayani Bagamoyo,ambapo aliambatana na uongozi wa mamlaka ya maji na usafi na maji taka Dar es salaam (DAWASA).(picha na Mwamvua Mwinyi)

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
UJENZI wa mradi wa tanki kubwa la maji linalojengwa Bagamoyo ,mkoani Pwani ambalo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi lita milioni sita linatarajiwa kuondoa tatizo la ukosefu wa maji kwenye wilaya hiyo na maeneo jirani.
Pamoja na hilo, mradi wa kusambaza maji kwenda wilaya ya Kisarawe kutokea kwenye chanzo cha Ruvu Juu na kusambaza maji kwenye baadhi ya maeneo ya Chalinze ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa maeneo hayo.
Hayo aliyaeleza mkuu wa Mkoa wa Pwani,mhandisi Evarist Ndikilo ,baada ya kutembelea baadhi ya miradi ukiwemo ule wa kupeleka maji kwenye eneo la uwekezaji na ujenzi wa tenki kubwa la kuhifadhia maji wilayani Bagamoyo,ambapo aliambatana na uongozi wa mamlaka ya maji na usafi na maji taka Dar es salaam (DAWASA).
Alielezea utatuzi wa kero ya maji unakwenda kupungua kama sio kubakia historia.
"Miradi hii itasaidia kuongeza idadi ya wananchi wanaopata huduma ya maji safi mkoani hapa kwani kwa sasa mijini ni asilimia 62 na vijijini ni asilimia 52 " #
"Miradi hiyo italeta ukombozi kwa wananchi ambao hawapati huduma ya maji kwa uhakika kutokana na changamoto mbalimbali " alifafanua Ndikilo.
Kuhusu kupeleka maji kwenye eneo la uwekezaji la EPZA alielezea ,liko umbali wa kilometa tano toka chanzo cha maji na tayari mabomba yenye ukubwa wa nchi 16 yameshatandazwa umbali wa kilometa 2.7 zikiwa zimesalia kilometa 2.3 ambako ndiko kutakakojengwa bandari mpya.
Ndikilo alisema, DAWASA wanapaswa kuwasimamia wakandarasi ili wakamilishe miradi kwa wakati na kuwaondolea wananchi kero ya kukosa maji.
Mkuu huyo wa mkoa ,alisema,serikali inaendelea na jitihada za kupunguza tatizo la maji na  kuweka miundombinu wezeshi kwenye maeneo ya uwekezaji.
“Asilimia 88 ya maji yanatoka mto Ruvu hivyo kuna haja ya kuwazuia watu wanaofanya shughuli kandokando ya mto ikiwa ni pamoja na kuchunga mifugo na kilimo,";  Watumie sheria ya kutofanya shughuli za kilimo ndani ya mita 60,” alisisitiza Ndikilo.
Nae meneja miradi wa DAWASA mhandisi Lydia Ndibalema ,alisema kuwa watawasimamia wakandarasi hao ili kukamilisha miradi hiyo kwa wakati lengwa .

Ndibalema alisema wamejipanga vema kuhakikisha miradi hiyo inakuwa na manufaa kwa wananchi ili kuondokana na changamoto za ukosefu wa maji kwenye maeneo ya miradi hiyo.

Post a Comment

0 Comments