Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa(kushoto) akisikiliza maelezo jana ya Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Tabora, Mhandisi Damian Ndabalinze (wa pili kutoka kulia) mara baada ya kukagua kipande cha barabara Tabora hadi Nyahua kwa ajili ya kujionea wizi wa alama za barabarani na eneo lililokarabatiwa la Nyahua kutokana na uharibifu uliosababishwa na maji ya mvua ya kukata mawasiliano baina ya Itiga na Tabora.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa( wa pili kushoto) alichungulia jana mkondo wa maji katika eneo la Nyahua yaliyosababisha kipande barabara katika eneo la Nyahua wilayani Uyui kukatika na kusababisha mawasilano baina ya Tabora ya Itigi kukatika. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Tabora, Mhandisi Damian Ndabalinze .
_ Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa(kushoto) akitoa maelekezo jana katika eneo la Nyahua wilayani Uyui kwa Mwakilishi wa Kampuni ya CHICO Peng Hao (kulia) mara baada ya kutembelea eneo la barabara ya Itigi hadi Tabora lililoharibiwa na maji ya mvua.
Picha na Tiganya Vincent
RS TABORA



0 Comments