NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
SERIKALI
imetangaza kutoa zawadi nono kwa wananchi watakaosaidia kutoa taarifa
za siri za kuwafichua watu wanaong’oa alama za barabarani na
kuisababishia hasara kutokana na urejeshaji wake.
Kauli hiyo ilitolewa Machi 23, 2018 na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa mara baada ya kukagua
ukarabati wa eneo Nyahua ambalo lilikuwa limekatika kutokana na maji ya
mvua yaliyopelekea kukosekana kwa mawasiliano baina ya Itigi na Tabora
jana wilayani Uyui.
Alisema
Serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi kuweka alama za barabara ili
kuwaongoza watumiaji wa barabara kuepuka ajali lakini baadhi ya watu
wamekuwa wakihuju na kung’oa alama hizo kwa ajili ya kwenda kuziua kama
vyuma chakavu.
Kwandikwa
alisema mtu atakayesaidia kutoa siri ya wanaong’oa alama hizo na
wanunuzi wake atapewa zawadi na jina lake halitafichuliwa kwa ajili ya
usalama wake.
Alisema
inasikitisha kuona kuwa alama zipatazo 78 zenye thamani ya shilingi
milioni 27 katika kipande cha barabara ya urefu kilometa zipatazo 80.6
kutoka Tabora hadi Nyahua zimeng’olewa.
Naibu
Waziri huyo alisema alama hizo zinatumia fedha nyingi za Serikali kwa
kuwa baadhi yake zinatoka nje ya nchi na kuongeza kuwa vitendo hivyo ni
hatari sana ni vema wahusika wakikamatwa washitakiwe kama wahujumu
uchumi.
Alisema
hata pale Serikali ilipoamua kujengwa alama hizo kwa Sementi bado
baadhi ya watu wamekuwa wakizivunja ili kutoa nondo zilitumika katika
ujenzi wake.
“Fikiria
katika muda wa siku moja alama zaidi ya moja alama za barabarani 30
mkoani Kilimanjaro zimeng’olewa … Je? Kwa mwezi ni alama ngapi
zinang’olewa ..pesa ngapi za Serikali inapotea kurudisha alama hizo …Ma
RC na Ma DC na wananchi saidieni katika kupambana na wahujumu wa
miundombinu katika maeneo yenu” alisema Kwandikwa.
Aidha
Naibu Waziri huyo alisema hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wauzaji na
wanunuzi wa vyuma chakavu watakoa patikana na alama za barabara ili iwe
fundisho kwa watu wanohujumu miundimbinu.
Kwandikwa
alisema jamii inawajua vema wanaonunua vyuma chakavu ni vema wakatoa
taarifa za siri ili kukomesha tatizo hilo ambalo limekuwa likichangia
sehemu ya ajali nyingine za barabarani.
“Meneja
wa TANROADS nafikiri tuanze kutoa kiasi fulani cha fedha kwa mtu
anayetusaidia kutoa taarifa za siri kwa watu wanaong’oa alama za
barabarani ili tukomesha tatizo” alisema Naibu Waziri.
Hivi
karibuni Kamati ya Kudumu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ikiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani Tabora ilielezea kusikitishwa
kwake na wizi wa alama za barabarani katika barabara nyingi za Mkoa huo
na kuagiza viongozi wa maeneo husika ambapo barabara kuu zinapita
wasimamie ulinzi.

0 Comments