Klabu ya Simba inatarajia kucheza
mchezo wake wa Kombe la Shirikisho dhidi ya klabu ya Al Masry kutoka
nchini Misri siku ya Jumatano ya tarehe 7/3/2018 katika uwanja wa Taifa
Jijini Dar es salaam.
Mchezo huo unatarajiwa kuanza
mishale ya saa 12 kamili jioni, Aidha viingilio katika mchezo huo
vinataraji kuwa katika bei zifuatavyo;-
- VIP A – Tsh 20000
- VIP B – Tsh 15000
III. Mzunguko/Orange – Tsh 5000.
Tiketi za kuingilia uwanjani siku
hiyo zitaanza kuuzwa siku ya Jumatatu kwa mawakala wa Selcom na vituo
vitakavyotangazwa hapo baadae.
Klabu inawaomba mashabiki na
wapenzi wa klabu kujitokeza kwa wingi siku hiyo kuishangilia timu yao
itakapokuwa inacheza, aidha inawakumbusha kununua tiketi za mechi hiyo
kwa wakati.
Katika hatua nyingine,Klabu ya Al
Masri inataraji kuwasili nchini siku ya Kesho Jumapili majira ya saa 12
jioni,na itafanya mazoezi siku ya Jumatatu jioni katika Uwanja Taifa.
Pia,waamuzi wa mchezo huo kutoka nchini Afrika kusini wanatarji kuwasili nchini siku ya Jumatatu saa 10 jioni.
Imetolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano,
Simba Sports Club,
Haji S. Manara
3/3/2018
Simba Nguvu Moja..!!!

0 Comments