Na WAMJW-Dodoma.
Kifua Kikuu(TB) ni ugonjwa wa
kuambukiza unaoongoza kwa kusababisha vifo vingi Duniani.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika
la Afya Duniani(WHO) inakadiriwa kuwa zaidi ya watu milioni 10.4 huugua Kifua
Kikuu kila mwaka Duniani na Milioni Moja kati ya hao ni watoto wenye umri chini
ya miaka 15.
Tafiti nyingi zinaonesha kuwa
karibia theluthi moja ya Watanzania tayari wamepata maambukizo ya Kifua Kikuu
na wanaishi na vimelea mwilini mwao.
Kauli mbiu ya mwaka huu inasema
*” Viongozi Tuwe Mstari wa Mbele Kuongoza Mapambano ya Kutokomeza TB.”*
Nchini Tanzania kila mwaka jumla
ya watu 160,000 wanakadiriwa kuwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu.
Nitoe wito kwa viongozi wa ngazi
zote kuifanya vita dhidi ya TB kuwa agenda muhimu na ya kipaumbele.
Napenda kuwakumbusha TB inatibika
na kupona kabisa, dawa zake zinatolewa bure na zinapatikana sehemu zote nchini
katika vituo vya Umma na Binafsi.
Serikali imechukua hatua
mbalimbali kukabiliana na tatizo la Kifua Kikuu nchini ikiwemo kuimarisha
uchunguzi na ugunduzi wa Kifua Kikuu katika Vituo vya Afya.
Pia Serikali imezindua dawa mpya
za TB za watoto ili kuhakikisha zinakidhi matakwa ya Shirika la Afya Duniani (
WHO), dawa hizo mpya ni za watoto za mseto ( RHZ/RH) zilizoboreshwa na
tayari zimeshawasili nchini na tumeanza kuzisambaza kwenda Mikoani na
Halmashauri zote nchini.
Nawaagiza waganga wafawidhi wote
wa hospitali na vituo vya huduma kuhakikisha watoto wote wanaoanza shule za
bweni wanafanyiwa uchunguzi wa TB kikamilifu kabla ya kuanza masomo.
Ni marufuku kwa Madaktari
kujaza fomu za uchunguzi wa Afya bila kupima wanafunzi husika. Kufanya
hivyo ni kuliangamiza kwa makusudi Taifa kwa uzembe ambao hauwezi kuvumilika.
Serikali inatambua umuhimu wa
ushirikishwaji wa jamii katika mapambano ya kutokomeza TB.
Mpaka sasa takribani watoa
huduma1530 kati ya 5000 katika ngazi ya jamii ambao wamepata mafunzo ya muda
mfupi ya Kifua Kikuu wanawezeshwa ili kuibua wagonjwa wa TB na kuwafuatilia
watoto wanaopata matibabu katika maeneo yao.

0 Comments