Random Posts

Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Watembelea Eneo la Ujenzi wa Ofisi za Nec Dodoma

 Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage wakimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Ujenzi wa jengo la NEC kutoka TBA, Mhandisi Yohana Mashausi (kushoto) walipotembelea eneo la Mradi wa Ujenzi wa Jengo hilo eneo la Njedengwa mkoani Dodoma.
 Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage wakiendelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la NEC mkoani Dodoma. Wajumbe hao wameitaka TBA kukamilisha mradi huo kwa wakati.
 Sehemu ya jengo la Utawala la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zinazoendelea kujengwa eneo la Njedengwa mkoani Dodoma.
Msimamizi wa Mradi kutoka Chuo Kikuu Ardhi, Godwin Maro akitoa taarifa ya maendeleo ya Ujenzi wa Ofisi za Tume kwa Wajumbe na Menejimenti ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi waliotembelea eneo
la mradi mkoani Dodoma.
Picha na NEC

Post a Comment

0 Comments