Mmoja wa watoto wa wafugaji, kijiji cha Eworendeke, kata ya Kimokouwa,
Wilayani Longido akipata maziwa kwa ajili ya matumizi yake kwa kukamua bure
mbuzi waliofikishwa muda wa jioni katika Soko la kimkakati la
mifugo Longido kuuzwa, Soko hilo, limejengwa na Programu ya Miundo mbinu ya
Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).
Baadhi ya watoto wa
wafugaji, kijiji cha Eworendeke, kata ya Kimokouwa, Wilayani Longido wakipata
maziwa kwa ajili ya matumizi yao kwa kukamua bure mbuzi waliofikishwa
muda wa jioni katika Soko la kimkakati la mifugo Longido kuuzwa, Soko
hilo limejengwa na Programu ya Miundo mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na
Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).
Mmoja wa watoto wa wafugaji, kijiji cha Eworendeke,
kata ya Kimokouwa, Wilayani Longido akipata maziwa kwa ajili ya matumizi yake
kwa kukamua bure mbuzi waliofikishwa muda wa jioni katika Soko la
kimkakati la mifugo Longido kuuzwa, Soko hilo, limejengwa na Programu ya Miundo
mbinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF).
Katika
kijiji cha EWORENDEKE, kata ya KIMOKOUWA, Wilayani LONGIDO mkoani ARUSHA,
kijiji hicho kipo takriban kilomita 4 kutoka Namanga, mpaka wa Tanzania na
Kenya.
Hapo
kuna Soko la
Kimkakati la mifugo Longido, linalohusika
na uuzaji wa mifugo kutoka mikoa
takribani 7 ya hapa nchini Tanzania. Wafugaji huuza mifugo hiyo hapa nchini na
nchi za jirani, soko hilo ambalo limejengwa na Programu ya Miundo mbinu ya
Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), limekuwa
ni neema kwa watoto wa kaya zinazozunguka soko hilo.
Watoto wa wafugaji wa jamii ya kimaasai ambao ndiyo wanufaika wa
soko hilo wameguswa na uwepo wa soko hilo kwa kupata maziwa ya mbuzi bure. Watoto
hao hukamua maziwa hayo kutoka kwa mbuzi ambao hufikishwa sokoni hapo muda wa jioni
na kusubiri kuuzwa usiku ambapo mnada wa mifugo kwa wafanyabiashara wa ndani na
nje ya nchi hufanyika sokoni hapo.
Mratibu wa Kitaifa wa Program ya
MIVARF,Walter Swai, amebainisha kuwa tangu Program hiyo ianzishwe kutekelezwa rasmi mwaka 2011, katika mikoa yote ya
Tanzania bara na Zanzibar imekuwa ikichochea faida nyingi, zaidi ya malengo mahususi
yaliyokusudiwa na Program ambayo, ni kufanikisha azma ya
Serikali ya Tanzania ya kuongeza kipato
kwa wananchi pamoja na uhakika wa
chakula kwa kaya zenye kipato cha chini hususan maeneo ya vijijini.
“’Kuna maeneo tumejenga barabara za vijijini hasa
kutoka maeneo ya uzalishaji, lakini tumekuta katika maeneo hayo ardhi imepanda
thamani, hivyo hivyo katika soko la Kimkakati Longido tayari tunaona hata akina mama wameanza biashara ya mama lishe lakini na
watoto wao wanapata maziwa ya mbuzi bure kwaaajili ya lishe yao” alisema Swai.
Mwenyekiti
wa wafanyabiashara wa Mifugo wilayani Longido, Saruni Laizer amesema kuwa hayo
ni mojawapo ya manufaa ya soko hilo lililojengwa
na Program ya MIVARF, kwani watoto wao wanakuwa na afya bora kwa kunywa maziwa ya mbuzi ambayo huyapata bure na
kisha huyachemsha na kuyatumia kwa matumizi ya nyumbani.
Soko hilo litawanufaisha
wananchi wapatao 14,2000 wa wilayani Longido ambapo asilimia 95 ni
wafugaji na wanaojishughulisha na biashara za mifugo, pamoja na kuwa wafugaji
ni walengwa wa Program hiyo , walengwa wengine ni wakulima wadogo, wavuvi na
wafanyakazi wa kazi za mikono (artisans), Wajasiriamali na wafanyabiashara
wadogo walioko vijijini.
MIVARF; ni Programu ya
Miundo Mbinu ya Masoko na Huduma za Kifedha Vijijini iliyobuniwa na
serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Mfuko wa Kimataifa wa
Maendeleo ya Kilimo yaani (IFAD) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB). Dhumuni la kuanzishwa
kwa Programu ya MIVARF ni; Kuboresha miundo mbinu ya
masoko, barabara za vijijini, maghala na masoko, Kuwawezesha wananchi waishio
vijijini na kuongeza thamani mazao ya
kilimo.



0 Comments