Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa. Katikati mwenye tai akikagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (JNIA), Jijini Dar es Salaam,leo March 23/2018 .Kushoto kwa Waziri Mkuu
ni Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda na kulia ni Msimamizi wa Mradi. Eng.
Julius Ndyamukama .
PICHA NA OFISI YA
WAZIRI MKUU
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea
mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kwamba ameridhishwa na maendeleo yake.
Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia
asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika Juni 2019 na utakuwa na uwezo wa kuegesha
ndege kubwa 24 kwa wakati mmoja, pamoja na kuhudumia abiria milioni sita kwa
mwaka na kuwa na.
Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi
huo leo (Ijumaa, Machi 23, 2018) amesema amefarijika na maendeleo ya ujenzi wa
mradi huo pamoja na kukuta Watanzania wengi wakishiriki katika kazi za ujenzi.
“Serikali imejiimarisha katika
kuboresha usafiri wa anga, ambapo kukamilika kwa jengo hili kutachangia
ongezeko la ndege kubwa nyingi kutua nchini. Pia sekta ya utalii nayo
itaimarika kwa kuwa watalii wanaoingia nchini wataongezeka.”
Amesema mbali na ujenzi wa jengo hilo, pia Serikali
inaendelea kuvikarabati viwanja mbalimbali vya ndege nchini kikiwemo cha Musoma,
Iringa, Kilwa Masoko, Lake Manyara, Lindi, Moshi, Njombe, Tanga, Simiyu,
Singida na Songea ili kuboresha huduma za usafiri wa anga nchini.
Akisoma
taarifa za ujenzi wa mradi Mkurugenzi wa Miradi wa TANROADS, Mhandisi Christianus
Ako amesema mradi huo umeajiri wafanyakazi 1,400 kwa sasa na wanatarajia
kuongeza watumishi na kufikia 1,800.
Pia wanatarajia
kufanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa vya umeme kuanzia Julai, 2018
kwa kuwa tayari utekelezaji wa kazi kubwa za ujenzi wa mradi huo zimefanyika.
IMETOLEWA NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA,
MACHI 23, 2018.

0 Comments