Chama cha mapinduzi CCM
wilaya ilala kimewapa Pole wananchi wote waliopata athari za maafa
kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha, jijini Dar es salaam.
Taarifa hiyo imetolewa na
katibu mwenezi wa chama hicho wilaya ya Ilala Said sidde na ambapo
ametoa wito kwa viongozi wa chama ngazi zote kutoa ushirikiano wa kutosha kwa
waathirika, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo yao na kutoa msaada wa Hali na
Mali.
Aidha ameongeza kuwa misaada hiyo ni pamoja na njia za
kuwahifadhi waathirika hususan wanawake, watoto, wazee pamoja na wasiojiweza kwa
kushirikiana na viongozi wa serekali za mtaa.
"tutumie nafasi
yetu kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa na serikali kuu kufahamu
kiwango cha uharibifu wa Mali na miundombinu pamoja na takwimu za
walioathirika"alisema sidde.
Hata hivyo amewataka watu wote kushirikiana kumuombe
mwenyezi mungu kwa imani zao ili kupate
mvua za wastani zisizo na madhara kwa binadamu, mifugo na Mali.

0 Comments