Mbunge
wa jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi akiongea na baadhi ya wananchi
waliokuwa wamehudhuria katika hafla ya kukabidhi vifaa na gari la
kubebea wagonjwa kwa lengo la kuendelea kuboresha sekta ya afya katika
jimbo hilo
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi akikabidhi vitanda kwa ajili ya kituo hicho
Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini, Cosato Chumi akikabidhi gari la kubebea wagonjwa kwa ajili ya kituo hicho 



NA FREDY MGUNDA, MUFINDI
MBUNGE
wa Mafinga Mjini, Cosato Chumi ametoa msaada wa vitanda kumi kwa kituo
cha afya cha Ihongole kilichokuwa kinakabiliwa na upungufu wa vitanda
katika wodi ya wazazi.
Akizungumza
wakati kukabidhi vitanda hivyo sambamba na kukabidhi gari ndogo ya
kubebea wagonjwa iliyotolewa na serikali, Chumi alisema kuwa msaada huo
wa vitanda utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza changamoto katika kituo
hicho cha afya ambacho kinachohudumia wakazi zaidi ya 20000 wa jimbo la
Mafinga mjini.
Alisema
kuwa ushirikiano katika kuondoa changamoto na kuchukulia mapungufu ndio
njia pekee ya kuendelea kuinyanyua Mafinga hasa katika sekta ya afya
ambayo imekuwa ikikabiliana na changomoto nyingi.
Chumi
alisema kuwa msaada wa vitanda vimetolewa na mmoja wa wahisani
wanaolisaidia jimbo la Mafinga kuondokana na changamoto mbalimbali
katika sekta ya afya ambayo imekuwa na ikikabiliwa na mapungufu
mbalimbali ikiwemo ukosefu wa miundo mbinu bora.
Alisema
changamoto za sekta ya afya katika jimbo hilo na wilaya ya Mufindi kwa
ujumla zitakashughulikiwa kupitia serikali na wadau wake mbalimbali
wanaotakiwa kujitokeza kuboresha huduma zake
Akizungumzia
Gari hiyo ambayo imetolewa na Serikali Chumi alisema kuwa itatumika
kubeba wagonjwa ambao watalazimika kukimbizwa kwenye Hospitali ya
Mafinga ambapo awali ilikuwa vigumu kwa wagonjwa pindi wakizidiwa kwenda
kutibiwa.
Mbali
na msaada huo, mbunge huyo ambaye mbali na ahadi mbalimbali kwa wapiga
kura wake, aliahidi kuboresha huduma za afya katika jimbo hilo
amekwishatoa msaada vitanda, magodoro, viti vya kubeba wagonjwa na vifaa
tiba mbalimbali katika hospitali ya Mafinga.
Akipokea
na kushukuru kwa msaada huo, Kaimu Mganga Mkuu wa kituo cha Ihongole,
Bernad Makupa alisema msaada huo wa vitanda na gari ya kubebea wagonjwa
utasaidia kwa kiasi kikubwa kuwahudumia wananchi katika vijiji
mbalimbali vinavyopata huduma katika kituo hicho.
Kwa
niaba ya halmashauri ya Mafinga Mjini, mwenyekiti wa halmashauri hiyo,
Charles Makoga alimshukuru Chumi kwa ushiriki wake katika kuchangia
maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo kabla na baada ya kuingia madarakani
na akamuomba endelee na moyo huo.



0 Comments