Na Florah Raphael.
Mfumko wa bei wa
taifa kwa mwezi machi, 2018 umepungua hadi kufikia asilimia 3.9
ikilinganishwa na asilimia 4.1kama ilivyokuwa mwezi February, 2018.
Hayo yamesemwa leo na
Mkurugenzi wa sensa na takwimu za jamii, Ephraim Kwesigabo alipokuwa
akiongea na vyombo vya habari kuhusu mfumuko wa bei wa taifa katika
ofisi ya taifa ya takwimu.
Kwesigabo amesema
kuwa kupungua kwa mfumko wa bei inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya
bei za bidhaa na huduma kwa mwaka uloishia mwezi machi, 2018 imepungua
ikilinganishwa na kasi ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia februari, 2018.
Aidha amesema kuwa
kupungua kwa mfumko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi machi,2018
kumechangiwa hasa na kupungua kwa mfumko wa bei za vyakula na baadhi ya
bidhaa za vyakula zilizochangia kupungua kwa mfumuko wa bei kati ya
machi, 2017 na machi,2018 ni pamoja na mtama kwa 7.1%, unga wa mihogo
6.7%, maharage 3.9%, mihogo mibichi 16.6% na ndizi za kupika 16.7.
Pia amesema kuwa
mfumuko wa bei kwa baadhi ya nchi za Afrika mashariki ni kama ifuatavyo
Uganda mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia machi,2018 umepungua hadi 2.0%
kutoka 2.1% kwa mwaka ulioishia mwezi februari, 2018 na kwa upande wa
Kenya mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi machi,2018 umepungua hadi
4.18% kutoka 4.46% kwa mwaka ulioishia mwezi februari, 2018.

0 Comments