Meneja Uendeshaji wa MultiChoice
Tanzania Baraka Shelukindo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo maalum cha
huduma jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Kanda John Kasuku.
Meneja
Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Baraka Shelukindo akitoa maelezo kuhusu kituo
maalum cha huduma jijini Mwanza mara tu ya ufunguzi wa kituo hicho mwishoni mwa
wiki.
Menejawa
Kanda ya Ziwa wa MultiChoice Tanzania John Kasuku (kulia) akimkabidhimuandishi
wa habari George Ramadhani seti ya DStv baada ya muandishi huyo kuwa miongoni mwa waandishi waliojishindia seti ya DStv wakati
wa uzinduzi wa kituo kipya cha huduma jijini Mwanza mwishon mwa wiki.
..........................
Katika kuhakikisha
kuwa inaimarisha na kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja, kampuni ya
MultiChoice Tanzania imefungua kitua kipya cha huduma jijini Mwanza.
Kituo hicho
kilichofunguliwa mwishoni mwa wiki ni muendelezo wa mkakati wa kampuni hiyo
kuwasogezea wateja wake huduma karibu ambambo hivi karibuni, kituo kama hicho
kilifunguliwa mlimani City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa
ufunguzi huo, Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Baraka Shelukindo
amesema kituo hicho ni cha Kisasa na kinaweza kuwapa wateja wa DStv huduma zote
kuanzia kununua vifaa, kufanya malipo, ufundi na huduma kwa wateja.
Amesema huu ni mkakati
maalum wa MultiChoice Tanzania kufungua vituo kama hivyo kote nchini ambapo
hivi karibuni vituo zaidi vitafunguliwa katika miji ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha na Dodoma.
Hivi sasa mkakati wetu
mkubwa ni kuhakikisha kuwa mteja aliyeko mkoani anapata huduma sawasawa na yule
aliyepo Dar es Salaam kwani vituo hivi vya huduma vimeboreshwa na kuwa na uwezo
wa kutoa kila aina ya huduma alisema Shelukindo.
Amewataka wateja wa
DStv jijini Mwanza kukitumia kituo hicho kwa ufanisi na pia sasa kampuni hiyo
pia inaimarisha timu yake ya mauzo, kuongeza idadi ya mawakala ili kuhakikisha kuwa wateja wanahudumiwa kwa haraka na
kwa ufanisi mkubwa.
Kuhusu changamoto za
kiufundi, Shelukindo amesema hili sasa limepatiwa ufumbuzi kwani MultiChoice
imetoa mafunzo maalum ya ufundi kwa mamia ya vijana kote nchini kwa ajili ya
kuwahudumia wateja wake.
Amesema kuanzia sasa
kutakuwa na mafundi maalum walioidhinishwa ambao wamepatiwa mafunzo maalum.
0 Comments