Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege (kushoto)
akiwapokea wajumbe wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa toka Nchini Uganda
waliotembela Wizara kuona ubora wa miradi ya Benki ya Dunia inavyotekelezwa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa toka
Uganda (PAC-LG) Mhe. Ronald Reagan Okumu (kulia) akiwa na mjumbe wa Kamati hiyo
toka Uganda wakifuatilia kikao na Naibu Waziri wa Tamisemi(hayupo pichani) Mhe.
Joasephat Kandege.
Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe. Josephat Kandege akifurahia jambo
wakati wa kikao cha Mapokezi ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa.
Wataalam wanaosimia Miradi ya Benki ya Dunia OR-TAMISEMI pamoja na
Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda wakimskiliza
mtaalamu wa maabara ya mradi wa DMDP.
Wataalam wanaosimia Miradi ya Benki ya Dunia OR-TAMISEMI pamoja na
Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa toka Uganda wakimskiliza
mtaalamu wa maabara ya mradi wa DMDP.
Kamati ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kutoka Nchini
Uganda (PAC-LG) imemwagia sifa Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam
unaoendelea kutekelezwa katika Manispaa ya Tano za Mkoa wa Dar es salaam.
Kamati hiyo yenye zaidi ya wajumbe kumi waliotemebelea Mradi wa DMDP
unaotekelezwa chini ya Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
wamesema ni mradi wa mfano na kuigwa na Nchi za Afrika Masshariki zinazopata
mkopo wa fedha kutoka Benki ya Dunia.
Akizungumza katika ziara hiyo ya mafunzo Mwenyekiti wa Kamati hiyo
(PAC-LG) Mhe. Ronald Reagan Okumu amesema lengo la ziara yao ni kuona namna
ambavyo miradi ya Uboreshaji Miundombinu inayotekelezwa kwa fedha za Mkopo toka
Benki ya Dunia;
“Tunapenda kuona ubora wa miradi hiyo, taratibu za ulipaji fidia
zilivyofuata, maelekezo ya mkopo wa fedha hizo yalivyozingatiwa na zaidi namna
ambavyo fedha zilivyopokelewa, zinavyosimamiwa na wataalamu, zinavyotumika na
zinafanyiwa ukaguzi na zaidi suala zima la thamani ya fedha”Value for
Money” kuonekana katika miradi hiyo” alisema Mhe. Okumu.
Akipokea ujumbe huo toka Bunge la Uganda Naibu Waziri Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege amesema
mradi huu umetekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu sasa na mafanikio
yaliyopatikana ni makubwa na kwa kiasi kikubwa umesaidia kuwapunguzia kero
wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam.
“Karibu mjifunze kwa kuona mtaona barabara zilivyojengwa kwa ubora
wa hali ya juu, njia za bora waenda kwa miguu, mifereji yenye viwango ya
kusafirishia maji ya mvua, masoko na ofisi za miradi pamoja na maabara za
kisasa za kupima ubora wa barabara zinazoendelea kujengwa “ alisema Kandege.
Akielezea Miradi inayotekelezwa chini ya fedha za Mkopo wa Benki
ya Dunia Mratibu wa Miradi hiyo toka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa Eng. Davis Shemangale amesema kuwa mradi huu unatekelezwa kwa
kipindi cha miaka mitano na unalengo la kuboresha Jiji la Dar es salaam
lizidi kuwa bora katika Sekta ya miundombinu, usafiri mjini pamoja na
usalama
Eng. Shemangale aliongeza
kuwa mradi huo pia utaboresha makazi bora sambamba na kujenga uwezo wa
Kitaasisi pamoja na mifumo stahiki na ya kutosha kutunza kumbukumbu na takwimu
itakayosaidia katika Ukusanyaji wa mapato.
Naye mratibu wa mradi wa uendelezaji wa Jiji la Dar es salaam
(DMDP) Eng. Emmanuel Ndyamukama amesema Katika awamu ya kwanza ya mradi
huu itagharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 300 ambazo ni Fedha za Mkopo
kutoka Benki ya Dunia. Aidha Shirika la maendeleo la Nchi za Nordic litatoa
ruzuku ya dola za kimarekani Mil. Tano kwa ajili ya kukabili changamoto za
mabadiliko ya Tabia ya Nchi na huku Serikali ya Tanzania ikichangia takribani
Dola za Kimarekani Mil. 25.3 kwa ajili ya kulipa fidia wananchi walioathirika na mradi.
Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa iko katika ziara ya
mafunzo kwa muda wa siku Tano na itatemebela miradi ya uendelezaji wa Jiji la
Dar es salaam (DMDP), Mabasi yaendayo haraka (BRT) kasha kuelekea katika
Manispaa ya Morogoro ambako watatembelea mradi wa uboreshaji na uimarishaji wa
Mamlaka za Miji (ULGSP) kasha kumalizia na Jiji la Dodoma ambako watajione
mradi wa Uboreshaji Miji Kimkakati (TSCP).
0 Comments