Baadhi ya
wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) na wa Tanzania Health Summit wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya shilingi milioni moja fedha ambazo
zitatumika kwa ajili ya kulipia gharama za matibabu ya upasuaji wa moyo kwa
mtoto Mbaruku Kabwe aliyelazwa JKCI kwa
ajili ya matibabu. Kushoto ni mama wa mtoto Asha Omary mkazi wa Gongo la Mboto
jijini Dar es Salaam.
Rais wa Tanzania Health Summit Dkt. Omary Chillo
akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof.
Mohamed Janabi hundi ya shilingi milioni moja kwa ajili ya kulipia gharama za
matibabu ya upasuaji wa moyo kwa mtoto Mbaruku Kabwe aliyelazwa katika Taasisi
hiyo kwa ajili ya matibabu. Kila mwaka Tanzania
Health Summit wanaandaa mashindano ya Heart Marathon lengo likiwa ni kusaidia watoto wanaosumbuliwa na magonjwa yasiyoambukiza ukiwemo ugonjwa wa
moyo.
Picha na JKCI


0 Comments