Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Heiko Maas, Ikulu jijini Dar es Salaam.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Heiko Maas wengine pichani kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga (kulia) na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Zanzibar Mhe. Issa Gavu, Ikulu jijini Dar es Salaam.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Heiko Maas mara baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Heiko Maas, Ikulu jijini Dar es Salaam.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Heiko Maas.
Makamu wa Rais amesema kwa pamoja wamekubaliana
kusaidiana katika kuleta utaalamu na teknolojia kwenye viwanda vyetu hapa
Tanzania haswa kwenye maeneo ya Kilimo, Uchimbaji Madini na Viwanda vya Madawa.
Makamu wa Rais asema Tanzania na Ujerumani wana Historia
ya miaka mingi hivyo wamekubalina pia kujenga uwezo kwenye mambo ya uhifadhi
ili kuvumbua mambo zaidi ambayo yapo Tanzania ili kukuza Utalii wa kuonyesha
mambo ya Tanzania na Historia yake.
Makamu wa Rais amewashukuru kwa msaada wa masuala ya Afya
haswa Afya ya Mama na Mtoto pamoja na uendelezaji wa shughuli za Utalii.
Makamu wa Rais aliwaomba tusaidiane katika kuzalisha
umeme zaidi hapa Tanzania na kuwataka pia kuleta wawekezaji Zaidi Tanzania na
wamekubalina hayo.
Kwa Upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la
Jamhuri ya Ujerumani Mhe. Heiko Maas alisema amefurahi kutembelea Tanzania na
ameisifia ni nchi nzuri sana na kuahidi kuendelea kwa Ushirikiano pamoja na
kuendelea kusaidia katika masuala mbali mbali ya kuleta maendeleo.




0 Comments