Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Tanga Lulu
George kulia akifutilia matukio mbalimbali kwenye mkutano huo kushoto ni
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Edwaed Bukombe 
WAANDISHI wa Habari Mkoani Tanga wametakiwa kuwajibika kwa kufanya kazi
kwa kufuata miongozo na maadili ikiwemo kuweka uzalendo mbele kwa ajili
ya maslahi ya nchi na jamii zinazowazunguka.
Hayo yalisemwa leo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga Mhandisi Zena Saidi
wakati akizungumza katika siku ya uhuru wa vyombo vya habari nchini
ambayo ilifanyika kimkoa kwenye ukumbi wa klabu ya waandishi wa Habari
Jijini Tanga.
Alisema iwapo watazingatia maadili na kuweka mbele uzalendo itasaidia
kuweza kuwasaidia kutangaza fursa mbalimbali za kiuchumi na maendeleo
kupitia vyombo vya habari ili viweze kupata mafanikio makubwa.
“Ndugu zangu niwaambie uhuru wa habari ukitumika vyema vyombo vya habari
vina mchango mkubwa kwa mkoa na nchi katika nyanja za kijamii, kiasiasa
na kiuchumi kwa kujenga jamii yenye kiu ya kuleta maendeleo “Alisema.
“Lakini pia amani na utulivu wa jamii ni muhimu zaidi kuliko vipato
vyote ...Gharama ya kurudisha amani ikivunjika ni kubwa kwa hiyo wote
tuna wajibu wa kuilinda kwa kauli zetu, vitendo vyetu na maandishi
yetu”Alisema.
Aidha alisema vyombo vya habari vina wajibu mkubwa kwenye jamii kwa
kupasha habari zenye ukweli,kujenga na kuleta matumaini kwa jamii hivyo
ni vema kuchuja na kuepuka habari zinazoleta migongano na mifarakano
katika jamii hata kama zinavutia na kuwapa vipato vya haraka.
Hata hivyo alisema vyombo vya habari ni kiungo muhimu kati ya uongozi wa
makali popote na jamii lakini pia maagizo, makatazo,fursa na taarifa
mbalimbali zitokazo kwa viongozi huwafikia wananchi kupitia vyombo vya
habari .
(Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
0 Comments