Random Posts

Warsha Endelevu wa Ishirini na Tisa ( 29 ) wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Kufanyika Mei 18-19, 2018 Jijini Dodoma.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Dkt.Ludigija Bulamile (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mei 10, 2018 kuhusiana na maandalizi ya  warsha ya siku mbili wa wataalamu wa ujenzi utakaofanyika Mei 18 mwaka huu Jijini Dodoma (katikati)  Kaimu Msajili wa Bodi hiyo   Albart Munuo (kulia) Mkuu wa Idara ya Ukaguzi wa Ndani wa Bodi hiyo Ezekiel Stephen.
 Kaimu Msajili wa Bodi hiyo ambao ndiyo waandaaji wa mkutano huo Albart Munuo akielezea kuhusiana na maandalizi ya warsha hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Dkt.Ludigija Bulamile akijibu maswali kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano huo.

 Picha zote na Philemon Solomon.


WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika warsha wa siku mbili wa wawataalamu wa ujenzi utakaofanyika Mei 18, 2018  Jijini Dodoma ambapo mada kuu itakuwa ni kujadili jukumu la Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi katika kuendeleza viwanda nchini.

Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam Mei 10, 2018 Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) Dkt.Ludigija Bulamile alisema kuwa warsha hizi zilianzishwa mwaka 2003 na hufanyika mara mbili kwa mwaka ambapo jumla ya wadau 6,143 wa sekta ya ujenzi wamenufaika na mafunzo hayo.

Alisema katika warsha hiyo  ni ya 29 wabunifu wa ndani na wadau wengine katika sekta ya ujenzi watajifunza namna ya kukabiliana na na mabadiliko ya sayansi na teknolojia pamoja na kubadilishana uzoefu wa kazi za kitaalamu kwa lengo la kuziboresha na kuwapa fursa wataalamu katika sekta ya ujenzi kupata nasaha kutoka kwa viongozi wa serikali

"Warsha hiyo pia ni kwa ajili ya kuwanoa wabunifu majengo,wasanifu wa ndani ya majengo pamoja na wakadiriaji Majenzi ili waweze  kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika sekta ya ujenzi,"alisema.

Aliongeza kuwa,mkutano huu utahudhuriwa na wataalamu mbalimbali wa fani hiyo wa nchini ambapo mada zilizochaguliwa zitawapa fursa wadau katika sekta ya ujenzi na kukumbushana masula mbalimbali ya kitaalamu.

Bulamile alizitaja baadhi ya mada zitakazojadiliwa kuwa ni pamoja na nafasi ya Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi katika sera ya serikali ya awamu ya tano ya Ujenzi wa Viwanda na nafasi ya wataalamu hao.

"Ujenzi wa viwanda ni sera ya serikali ya awamu ya tano,Wabunifu Majengo,Wakadiriaji Majenzi na Wataalamu wanaoshabihiana kuwa ni wadau wakubwa katika ubunifu na kusimamia ujenzi wa viwanda,hivyo warsha hii ni fursa kwa wataalamu kufahamu mbinu za kuendeleza ujenzi wa viwanda ili wananachi wapate majengo bora na kwa gharama nafuu,"alisema Bulamile,

Kwa Upande wake Kaimu Msajili wa Bodi hiyo ambao ndiyo waandaaji wa warsha hiyo Albart Munuo alisema warsha hii itasaidia makampuni ya wabubifu majengo na wakadiriaji majenzi kuwa na mipango endelevu ya kuendeleza vipaji kwa wakurugenzi wapya ili waweze kuendeleza makampuni kwa kutumia uzoefu na ujuzi ambao wameupata kutoka kwa wakurugenzi wao mahiri wanaostaafu.

Alisema Kufanya hivi kutaendeleza makampuni yao kukua kwa uendelezaji wa huduma bora ya kitaalamu hata pale waanzilishi wanapokuwa wamestaafu au hata kufariki,"alisisitiza Munuo pia aliongeza kuwa katika mkutano huo kutakuwa na mada ya wataalamu hao kujua umuhimu wa kutunza afya ikiwa ni pamoja na kufahamu maradhi ya moyo na jinsi ya namna ya matibabu yake,"alisema.

Aidha bodi inawaasa wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi Wahandisi na wadau wengine katika sekta ya ujenzi kushiriki kwa wingi katika semina hii muhimu ili kuwaongezea ujuzi na maarifa ya kuboresha utendaji kazi wao.

Hata hivyo Bodi inawaomba waajiri wote katika sekta ya umma na binafsi kufadhili kwa kuwalipia wataalamu wao ada ili waweze kushiriki warsha hiyo ambayo ni muhimu katika ujenzi wa taifa hasa kipindi hiki ambacho nchi inakwenda katika uchumi wa viwanda.

Post a Comment

0 Comments