Taswira ya Jengo la Wizara
ya Maji na Umwagiliaji jijini Dodoma kabla ya kazi ya kukamilisha ujenzi wa
mwisho ili lianze kutumika.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akiangalia baadhi ya vyumba vya jengo
litakalokua makao makuu ya wizara yake jijini Dodoma.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akikagua mazingira ya kazi jijini
Dodoma pamoja na Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi ya Na Nandhra Bw. Daman Singh Nandhra.
Katibu Mkuu, Wizara ya
Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akikabidhi mkataba mapema leo jijini
Dodoma kwa Mkurugenzi wa kampuni ya
ujenzi ya Na Nandhra Bw. Daman Singh Nandhra ili kuanza kazi itayofanyika
kwa miezi 12 .
Katibu Mkuu, Wizara ya
Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akiongea na baadhi ya wafanyakazi
walioshuhudia mkandarasi akikabidhiwa kazi ya kukamilisha jengo la wizara yao
lililopo jijini Dodoma.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara
ya Maji na Umwagiliaji inatarajia kuhamia katika jengo lake jipya jijini
Dodoma ndani ya miezi kumi na mbili (12)
kuanzia sasa. Jengo hilo lipo mtaa wa Posta na litagharimu kiasi cha shilingi
bilioni sita.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo amesema hayo wakati
akimkabidhi mkataba mkandarasi atakayefanya kazi ya umaliziaji wa jengo hilo,
ambalo lipo katika hatua za mwisho.
Prof.
Mkumbo amesema anaelewa wapo watumishi ambao wanafanya kazi katika majengo
tofauti, ila jengo hilo litakapokamilishwa wote watakua katika eneo moja, hivyo
wawe na subira na waendelee kufanya kazi kwa kasi zaidi.
Ameongeza
kuwa mkandarasi, kampuni ya ujenzi ya Na NDHRA, anatakiwa kufanya kazi bora na
katika kipindi kilichoainishwa katika mkataba bila kuchelewa.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano
Wizara ya Maji na Umwagiliaji
10.05.2018





0 Comments