Kampuni ya MultiChoice Africa
Limited imethibitisha uteuzi wa Wakurugenzi wawili ambapo Mtanzania Maharage
Chande, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
MultiChoice Tanzania anakuwa Mkurugenzi mpya wa kanda ya Afrika Mashariki na
Magharibi wa kampuni hiyo.
Uteuzi
huo uliotangazwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Africa Brand de Villiers, unabainisha kuwa Maharage
anachukua nafasi ya Stephen Isaboke, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika
Mashariki ambaye sasa anakuwa Mkuu wa masuala ya Mamlaka (Group Executive Head
of Regulatory). Uteuzi huu unaanza rasmi Juni 1, 2018
Afisa
Mtendaji Mkuu wa MultiChoice Africa Brand
de Villiers amesema kuwa uteuzi wa Maharage
umezingatia upeo na uwezo wake mkubwa aliouonyesha katika kipindi alipoiongoza
MultiChoice Tanzania tangu alipojiunga na kampuni hiyo mwezi Juni mwak 2016.
“Ninaamini kwa uwezo na uzoefu aliouonyesha Maharage katika kipindi kifupi cha
kuiongoza kampuni ya MultiChoice Tanzania ni dhahiri kuwa atakuwa na mchango
mkubwa katika kuimarisha safu yetu ya uongozi na kusaidia katika kuongeza mbinu
na ujuzi aliokuwa nao katika kuimarisha kampuni yetu na kuhakikisha tunaendelea
kutimiza matakwa ya wateja wetu kote Afrika”
Kwa
upande wake Maharage amesema amepokea uteuzi huo kwa mikono miwili na kwamba
bila shaka hayo ni matokeo ya jitihada kubwa zilizofanywa na yeye pamoja na
wafanyakazi wote wa MultiChoice Tanzania.
“Kwa hakika kaitika kipindi kifupi
tumekuwa na mafanikio makubwa sana – kuanzia katika kuongeza idadi ya wateja
wetu, kuimarisha huduma zetu na pia kuongeza kuchangia katika maendeleo ya
jamii na uchumi wa nchi yetu kwa ujumla.
Haya ni mafanikio tunayojivunia sisi
kama kampuni na tumeyafikia kwa jitihada, nidhamu na uchapakazi. Hivyo naamini
mafanikio haya ya Tanzania tunaweza pia kuyatumia kama chachu ya kuleta
mafanikio kwa Afika nzima”
Baadhi
ya wafanyakazi wa MultiChoice Tanzania wameonyesha Furaha yao kubwa kwa uteuzi
wa Mkurugenzi huyo na kusema kuwa katika kipindi chake ameleta mageuzi makubwa
katika kampuni hiyo ambayo yameleta mafanikio makubwa kwa kamppuni, wafanyakazi
na jamii kwa ujumla.
Mmoja
wa wafanyakazi wa kampuni hiyo Esther Mtei amesema wamefurahi kuona mkurugenzi
wao amekabidhiwa uongozi wa kanda na kwamba hii ni heshima kubwa kwa Tanzania
ndani ya kampuni ya MultiChoice Africa.
“Uteuzi wa Maharage kuwa mkurugenzi wa
kanda ni uthibitisho tosha kuwa Watanzania tunaweza kushika nyadhifa kubwa kama
hizi na pia tunaaminika. Tunaamini uteuzi huu utakuwa ni chachu kwa watanzania
kuongeza bidii katika shughuli zaokwani fursa kubwa zipo kila mahali”
Kabla ya kujiunga na
MultiChoice Tanzania mwaka 2016, Maharage alifanya kazi katika ngazi za juu za
uongozi katika makampuni mbalimbali ikiwemo ya simu za mkononi ya Vodacom,
Benki ya NBC na pia Ofisi ya Rais Maharage ana shahada ya
teknolojia ya mawasiliano (Bachelor degree in Electronics and Communication) ya
chuo kikuu cha Dar es Salaam na pia shahada ya juu ya uongozi wa biashara (Masters
in Business Leadership) ya chuo kikuu cha Afrika Kusini (UNISA).



0 Comments