NA TIGANYA VINCENT
RS TABORA
5 May 2018
SERIKALI Mkoani Tabora imeagiza kusimamishwa
mara moja ujenzi wa vyumba vitatu vya madarsa katika Shule ya Msingi Ilolangulu Wilayani Uyui hadi
hapo ukaguzi maalumu wa fedha zilizotumika kujenga zinalingana na zinalingana
na michango iliyotolewa na wananchi ya milioni 11.
Agizo hilo limetolewa jana Wilayani Uyui na
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri wakati wa ziara yake katika maeneo mbalimbali
kwenye kampeni kupambana na utoro na kukagua miradi ya ujenzi wa vyumba vya
madarasa unafanywa na wananchi kwa kushirikiana na wadau wengine.
Alisema kuwa ameamua kuzuia kwa muada wa siku
ujenzi wa madarsa hayo matatu hadi hapo atakapopata ufafunuzi wa kuridhisha juu
ya matumizi ya shilingi milioni 11 zilizochangwa na wananchi zilivyotumika hadi
kufikia madarasa hayo yalipofikia.
Mwanri aliongeza hatua hiyo itasaidia
kuhakikisha kiasi cha milioni 25 zilizotolewa na Equip T kupitia Serikali kuunga
mkono juhudi za wananchi zinatumika sahihi kukamilisha sehemu iliyobaki na
madarasa yatakayojengwa yawe yanalingana na thamani fedha iliyotolewa.
Alisema baada ya kukagua baadhi ya vifaa
vilivyonunuliwa kwa ajili ya ukamilishaji wa madarasa hayo vinaonekana chini ya
kiwango jambo linaloweza kusababisha kujengwa kwa madarasa ambayo hayana
viwango vizuri na kufanya fedha ionekana kutolewa nyingi lakini halingani na
thamani ya majengo.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa wa
Tabora amemwagiza Mkurugenzi wa Mteandaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega na
maeneo mengine kuhakikisha miradi inayojengwa kwa ajili ya wananchi ikiwemo ile
ya elimu inazingatia matakwa ya kitaalamu na izingatie athari za kimazingira
ili kuepuka usababishaji wa hasara kwa wananchi.
Mkuu wa Mkoa huo wa Tabora alilazimika kutoa tahadhari
hiyo baada ya kutembelea boma la Shule shikizi ya Mwaguguli katika Halmashauri hiyo
linalojengwa kwa nguvu za wananchi lakini limeanza kuonyesha nyufa hata kabla
haijakamilika.
Alisema
kabla ya kuanza kwa ujenzi wa boma lingine lenye vyumba viwili vya madarasa ,
ofisi moja ya walimu na matundu wanne ya vyoo kwa gharama ya milioni 62
zilizotolewa wa Equip –T kwa lengo kuunga mkono juhudi za wakazi ni vema
wakatuma mhandisi wa ujenzi, mkaguzi wa ndani , mtaalamu wa mazingira na wataalamu
wengine kuchunguza sababu zilizo za nyufa katika bomu la kwanza la shule tarajiwa hiyo.
Mwanri alisema hatua hiyo inalenga kujua kama
mipasuko hiyo inasababishwa na udongo wa eneo husika au kuna mchezo ulifanywa
na Mkandarasi ili hatua ziweze kuchukuliwa kwa ajili ya kuepusha hasara kwa
wananchi na kujiridhisha kama eneo hilo sio sehemu ya Hifadhi ya Mistu.
Kwa upande wa Katibu Tawala Msaidizi
anayeshughulikia Elimu Mkoa wa Tabora Suzzan Nussu aliwataka Wakurugenzi
Watendaji na Wasimamizi wa Miradi yote ya ujenzi wa madarasa kuzingatia mafunzo
na maelekezo waliyopatiwa ili kuepuka kuwa na majengo yaliyojengwa chini ya
kiwango na kujikuta katika matatizo ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Alisema kwa wale wanaotekeleza Mpango wa
Equip T ni vema wakazingatia maelekezo waliyopatiwa kuhusu ujenzi wa madarasa
na Ofisi.
Nussu aliongeza kuwa ni vema maeneo yote
ambayo wamepatiwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa wakajitahidi kufanya
haraka kukamilisha ili watoto waache kutembea umbali mrefu kwenda shule

0 Comments