Habari za Hivi Punde

6/recent/ticker-posts

Header Ads Widget

SERIKALI KUZICHUKULIA HATUA KAMPUNI ZA UJENZI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Arch.Elius Mwakalinga akifungua mkutano  Mkuu wa kwanza wa mwaka Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB)uliofanyika 15 oktoba 2020, katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB) Edwin Nnunduma akielezea mpango wa kusajili kampuni na wataalam katika sekta hiyo wakati wa mkutano  Mkuu wa kwanza wa mwaka Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB) uliofanyika 15 oktoba 2020, katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.  
Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi  (AQRB) Arch. Dkt Ludigija Bulamile akifafanua jambo wakati wa mkutano huo,
Wataalam wa sekta ya ujenzi wakiwa katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elius Mwakalinga (katikati kulia) akiwa katika picha ya pamoja  na watalaam wa sekta ya ujenzi wakati wa mkutano  Mkuu wa kwanza wa mwaka Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB uliofanyika 15 oktoba 2020, katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.  

PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON

 .............................................................

SERIKALI imesema  hadi kufikia januari mwakani itaanza kuwawajibisha kwa  kuzichukulia hatua Kampuni za ujenzi,  wabunifu  majengo na wakadiliaji majenzi ambao watakuwa hawajajisajili.

Akizungumza katika mkutano  Mkuu wa kwanza wa mwaka wa Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi(AQRB), Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elius Mwakalinga, alisema kuwa hadi kufikia januari 2021 wataalamu wote wa sekta ya ujenzi wanatakiwa kuwa  wamejisajili ili  kuhakikisha kwamba kila anayefanya shughuli hizo awe ni mtaalam na si kuwaachia wasio na taaaluma kufanya shughuli hizo.

“Hii ni taaluma muhimu na nyeti kwa uchumi wa nchi yetu, tuko katika ujenzi wa uchumi wa viwanda, na juhudi hii haiwezi kufikiwa katika malengo yake kama hakuna wataalam wa uhakika katika sekta hii, na ndiyo maana tunataka tuhakikishe wote wanasajiliwa na tunawatambua,”alisema Mwakalinga.

Alisema  tunataka shughuli zote  sifanywe na wataalam na siyo kuruhusu watu wasio sahihi kuvamia sekta hii na kuharibu, na usajili huu utarahisisha kuwatambua wavamizi na kuwachukulia hatua kali za kisheria. 

Lengo ni kuongeza udhibiti wa shughuli za wataalam wasiosajiliwa na kufanya kazi bila kuwa na leseni.”

Mwakalinga alisema pia kwa sasa serikali inaandaa mfumo maalum wa ufuatiliaji wa uendeshaji wa vivuko nchi nzima kwa kufunga vifaa maalum (GPS)ambavyo vitasaidia kurekodi uendeshaji wake.

Aliongeza kuwa pamoja na mambo mengine mfumo huo unalenga kudhibiti uharibifu wa miundombinu na kusaidia kupunguza ajali zisizo za lazima.

“Hatua hii ya kufunga GPS iko kwenye mchakato na tunatarajia kwamba mpaka Januari mwakani tutakuwa tumekamilisha. 

Mfumo huu utatusaidia pia kufahamu pale kivuko kinapozidisha mzigo au kufanya shughuli zake kinyume na taratibu, hata tukiwa ofisini tutakuwa tunaona,”alisema Mwakalinga.

Kwa upande wake, Msajili wa Bodi hiyo, Edwin Nnunduma, alisema mpango wa kusajili kampuni na wataalam katika sekta hiyo  utasaidia kupunguza malalamiko mengi ambayo wamekuwa wakipokea kutoka kwa baadhi ya wavamizi wa taaluma hiyo pale wanapoharibu kazi.

Nnunduma alisema hadi kufikia Septemba mwaka huu, bodi hiyo ilikuwa imesajili Wataalam 1,126 na makampuni ya kitaalam 381.

“Wakati bodi inaanza wataalam waliosajiliwa walikuwa 188 na makampuni ya kitaalam 53, ongezeko hili ni kubwa lakini ukilinganisha na na uhitaji wa huduma za wataalam nchini , idadi hii bado ni ndogo,”alisema Nnunduma.

Post a Comment

0 Comments