Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimuapisha Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb) kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa
na Michezo, katika hafla fupi iliyofanyika leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu
Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimuapisha Mhe. Pauline Philipo Gekul (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Utamaduni,
Sanaa na Michezo, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimuapisha Mhe. Eng. Kundo Endrea Mathew (Mb) kuwa Naibu Waziri wa Habari,
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini
Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimuapisha Jaji Jacob Casthom Mwatembela Mwambengele kuwa Mjumbe wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimuapisha Mhe. Magdalena Kamugisha Rwebangira kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi, leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akimuapisha Ndugu. Asina Abdallah Omar kuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,
leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Lugha Bashungwa (Mb)
wa kwanza kulia, Naibu Waziri Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.
Pauline Philipo Gekul (Mb), Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia
ya Habari Mhe. Eng. Kundo Endrea Mathew (Mb) Mjumbe wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Jacob Casthom Mwatembela Mwambengele, Mjumbe wa Tume ya Taifa ya
Uchaguzi Mhe. Magdalena Kamugisha Rwebangira na Mjumbe wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi Ndugu. Asina Abdallah Omar wakila kiapo cha Maadili ya
Utumishi wa umma mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar
es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,
akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Serikali mara baada ya kumuapisha Waziri,
Naibu Mawaziri katika Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo pamoja na Wajumbe
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo tarehe 24 Oktoba, 2021 Ikulu Jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiagana na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye
katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo
tarehe 24 Oktoba, 2021 mara baada ya Rais huyo wa Burundi Mhe. Ndayishimiye
kuhitimisha zira yake nchini na kurejea Burundi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza
na Mke wa Rais Evareste Ndayishimiye wa Burundi kwenye uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021
wakati Mhe. Ndayishimiye alipokua akiondoka kurejea Nchini Burundi baada ya
kukamilisha ziara yake leo tarehe 24 Oktoba, 2021. kulia ni Rais wa
Ndayishimiye wa Burundi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye wakiangalia
vikundi mbalimbali vya ngoma za asili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24 Oktoba, 2021 mara baada ya
Rais huyo wa Burundi Mhe. Ndayishimiye kuhitimisha zira yake nchini na kurejea
Burundi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
na Mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye wakati Rais
huyo wa Burundi akiagana na viongozi mbalimbali waliomsindikiza katika uwanja
wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 24
Oktoba, 2021 mara baada ya Rais huyo wa Burundi Mhe. Ndayishimiye kuhitimisha
zira yake nchini na kurejea Burundi
PICHA NA IKULU.

0 Comments