Katibu Tawala Msaidizi,Miundombinu wa
Mkoa wa Morogoro Mhandisi
Ezron Kilamhama akisalimiana na Kaimu Msajili wa Bodi ya AQRB Mkadiriaji
Majenzi Qs. Nyaswa Kalomo aliopowasili kufungua mafunzo endelevu ya wataalamu
wa Majenzi yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji
Majenzi (AQRB) mjini Morogoro ( kulia ) Msajili Msaidizi (Usajili na
Mafunzo) wa Bodi hiyo Qs. Mashaka Bundala, Mwenyekiti wa Bodi hiyo Arch. Dkt.
Ludigija Bulamile.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhfWUEGJ5LzwduRx0oUeRDLPSNlkzmN_tnD6QSaDyHbOP0xGQqcAFNEVP3Ck-583XRvY8kBfEPFmM2UNcDZ1VRZZ2YpzA5GFUze9uQeDk4yMFGix5X1m-3YLMWxCPhLD5ezUdETGeV0Ag9MERmBbeRK01Fktx5k5QNEIjPitpUakkHKhUswuDg0dwoBpm8/w640-h426/4.jpg)
...............................................
SERIKALI
imeziagiza Bodi zenye Mamlaka ya Usimamizi katika Sekta ya Ujenzi kuhakikisha
wataalamu wanaopewa dhamana ya
kutekeleza miradi ya Ujenzi wanazingatia sheria za Kodi Ili serikali iweze kupata mapato na Shughuli
za ujenzi ziendelee kutoa mchango katika
ukuaji wa uchumi
Akifungua
mafunzo endelevu ya wataalamu wa Majenzi yaliyoandaliwa na Bodi ya Usajili wa
Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi
(AQRB) mjini Morogoro Katibu Tawala Msaidizi,Miundombinu wa Mkoa huo Mhandisi
Ezron Kilamhama kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa alisema
katika baadhi ya miradi ya Ujenzi inayosimamiwa na kutekelezwa na
wataalamu wa ndani ukwepaji wa kodi umekuwa mkubwa kiasi cha kusababisha
malalamiko dhidi ya umahiri na ujuzi wa Kampuni za ndani
Alisema
kaguzi ambazo zimekuwa zikifanywa na
mamlaka za Usimamizi kwenye miradi yetu zimekuwa na mapungufu makubwa kwenye
ubora na gharama za miradi kuwa juu.
"Nimefurahia
sana kusikia katika mafunzo haya kutakuwa na mada ya Mapitio kuhusu uzingatiaji
wa masuala ya Kodi, mada hii itukumbushe uwajibikaji, ufuatiliaji na
uzingatiaji wa nidhamu ya kulipa Kodi
katika kuendeleza Sekta ya Ujenzi," Alisisitiza Mhandisi Kilamhama
Aliongeza
kuwa, kuhusu mada ya ulinganifu wa gharama za ushauri kwa mujibu wa sheria ya
AQRB na ya PPRA mada hii itadaidia kupata uelewa wa pamoja Juu ya ukokotoaji wa
ada za ushauri kwa kutumia sheria hizi mbili za AQRB na PPRA
Pia alisema kwenye mada ya Usimamizi wa miradi katika Tasnia ya Ujenzi Nchini Tanzania mada hii ni muhimu hasa wakati huu ambapo serikali na Sekta binafsi zinatekekeza miradi mingi ya Ujenzi ambayo imekuwa kichocheo Cha ukuaji wa uchumi Nchini
"Bila wataalamu wetu kusimania vyema miradi hii hatutaweza kupata matokeo yanayoendana na thamani ya uwekezaji unaofanywa na serikali kwa kushirikiana na Sekta binafsi,"alisema Mhandisi Kilamhama
Akifafanua
kuhusiana na
Changamoto mbalimbali zinazoikabili swkta hiyo ikiwemo ya baadhi ya Taasisi za umma zinavyotekekeza miradi ya Ujenzi kwa utaratibu wa kutumia wataalamu wa ndani ya Taasisi yaani 'Force Accaunt' isivyo sahihi serikali imeliona suala Hilo na kila mara viongozi wakuu wa serikali wamekuwa wakitolea maelekezo kuwa sheria ya ununuzi wa umma inayohutaji wataalamu watumike uzingatiwe
Alisema serikali itaendelea kushirikisha kikamilifu wataalamu wa ndani katika hatua zote za ujenzi katika miradi ya Ofisi za halmashauri na Manispaa,Majengo ya hospitali za Rufaa,Mkoa na Kanda pia Masoko makubwa ya Kusasa na miradi ya Ujenzi wa vitui vikubwa Vya mabasi ya masafa marefu unatekekezwa kwa kutumia wataalamu waliosajiliwa na bodi
Kwa
upande wake Kaimu Msajili wa Bodi ya AQRB
Mkadiriaji Majenzi Nyaswa Kalomo kwa niaba ya Msajili wa Bodi hiyo
aliiomba Serikali kuendelea kuajiri
wataalamu waliosajiliwa na bodi katika
ofisi zote za umma Ili kutoa miongozo ya ujenzi kwa waendelezaji wa
Majengo waliopo mjini na vijijini
Alisema idadi ndogo ya Wabunifu Majengo, wakadiriaji Majenzi, Wabunifu madhari na wataalamu wengine wa ujenzi unachangia kwa kiasi kikubwa taifa katika ushiriki wa miradi mbalimbali
"Kukosekana kwa sheria ya Majengo ,sheria hii Ina nanufaa mengi kwenye Tasnia ya Majengo sambamba na wataalamu kuhusika moja kwa moja kupanga,kubuni, kujenga na kutunza Majengo na mazingira kwa kuzingatia usalama na afya ya watu na Mali, kudhibiti ubora wa vifaa Vya Ujenzi matumizi Bora ya mifumo na miundombinu ya Maji, gesi, nishati, mwanga, upepo, joto na baridi ndani na nje ya jengo pamoja na kutunza mazingira
Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Ludigija Bulamile alisema mafunzo haya kwa wataalamu wa ujenzi ni muendelezo wa taratibu za Bodi ya AQRB katika kuwanoa wataalamu Ili kuwawezesha kupendana na mabadiliko ya teknolojia ya Ujenzi
"Uchaguzi wa mada umefanywa mahususi Ili kuwakumbusha wataalamu wetu umuhimu wa kusimaia miradi ya Majengo na mazingira katika utekelezaji wa kazi zao za kila siku,"alisema Dkt Ludigija na kuongeza kuwa mafunzo hayo ni Usimamizi wa Miradi katika Tasnia ya Ujenzi Tanzania ambayo utajadiliwa pamoja na mada ndogo zingine nne
Hata
hivyo alizitaja mada zingine zitakazo jadiliwa kwenye mafunzo hayo kuwa ni
pamoja na shugulikia madai na masuluhisho ya migogoro katika Tasnia ya Ujenzi
Nchini,Mapitio kuhusu uzingatiaji wa masuala ya Kodi na ulinganifu wa gharama
za ushauri kwa mujibu wa sheria ya AQRB na PPRA.
0 Comments