Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Profesa Pallangyo akizungumza wakati akitoa taarifa kwenye Mahafali ya 22 ya taasisi hiyo Kampasi ya Singida yaliyofanyika jana Novemba 22, 2024.
Na Mwandishi Wetu, Singida
TAASISI ya Uhasibu Tanzania (TIA) Kampasi ya
Singida imefanya jumla ya tafiti 15 na kuchapishwa katika majarida mbalimbali
ya ndani na nje ya nchi.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa
taasisi hiyo, Profesa William Pallangyo wakati akitoa taarifa kwenye Mahafali
ya 22 ya taasisi hiyo Kamapasi ya Singida Novemba 22, 2024 ambayo yaliwahusisha
wahitimu 1,477 wa Kampasi ya Singida, wakiwemo
wanawake 812 (sawa na asilimia 55) na wanaume 665 (sawa
na asilimia 45).idadi ambayo ni sawa na asilimia 13 ya
wahitimu wote 11,620 wa kampasi za Dar es Salaam, Mbeya,
Mtwara, Mwanza, Kigoma na Singida, kwa Mwaka wa Masomo 2023/2024.
Pallangyo alisema wahitimu hao waliotunukiwa
Cheti cha Awali walikuwa ni 399, Cheti 447, Stashahada 443, na Shahada
188 katika fani mbalimbali kuwa mahafali hayo yalifanyika sambamba na
uzinduzi wa program ya shahada ya uzamili uzinduzi ulifanywa na mgeni rami Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego.
Alisema ili kuendeleza na kutimiza malengo ya
Taasisi, Kampasi ya Singida imeendelea kufanya tafiti zinazolenga kutatua
changamoto mbalimbali katika jamii, hususan katika maeneo ya Uhasibu na Fedha,
Ununuzi na Ugavi, Rasilimali Watu, Maktaba, na Ujasiriamali.
“ TIA inaendelea kuboresha miundombinu ili
kuhakikisha ongezeko la wanachuo linakwenda sambamba na ubora wa huduma na
kueleza kuwa Kampasi ya Singida imepokea
kiasi cha Sh. za Kitanzania Bilioni 13.5 kupitia
Mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi kwa Vyuo vya Elimu ya Juu na kuwa fedha hizo ni
kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Taaluma.
Alisema jingo hilo litakuwa na vyumba vya
madarasa, kumbi za mihadhara, ofisi, vyoo maalumu kwa watu wenye mahitaji
maalum, na chumba cha kunyonyeshea na kuwa litakapo kamilika litakuwa na
uwezo wa kuchukua wanachuo 3,637 kwa wakati mmoja.
“Nitumie fursa hii kuishukuru Serikali yetu ya
Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan, kuwezesha kupatikana kwa fedha hizo, ambazo ni mkopo wa gharama
nafuu kutoka Benki ya Dunia,” alisema Pallangyo.
Profesa Pallangyo aliongeza kuwa katika
kuhamasisha shughuli za kijamii na kukuza uhusiano na jamii inayowazunguka,
Kampasi ya Singida imeanzisha mpango mkakati wa miaka minne (2023-2027) wa
kuboresha somo la Hisabati katika shule za sekondari za
Singida mpango unaoendeshwa na Mhadhiri Msaidizi Mary Kayanda na
kuwa kwa sasa unatekelezwa katika Shule ya Sekondari Mandewa.
Alisema TIA kupitia Kampasi ya Singida
inaendelea kuunga mkono jitihada za serikali za kuendelea kuimarisha sekta ya
elimu na uchumi kupitia mafunzo, utafiti na ushauri wa kitaalam.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego
ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia kwenye mahafali hayo aliwasihi wahitimu hao kutumia mitandao ya kijamii kama
jukwaa la kutangaza bunifu zao, kukutana na wateja na kueneza mawazo mapya
badala ya kupoteza muda mitandaoni kwa mambo yasiyokuwa na manufaa.
“ Mitandao hii inatoa fursa kubwa ya kujitangaza, kukuza
biashara, na kufikia mafanikio makubwa ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla,”
alisema Dendego.
Dendego aliwakumbusha wahitimu hao kwamba, taswira ya Chuo hicho imejengwa na wahitimu waliowatangulia hivyo popote watakapokuwa hasa kwa wale watakaosoma vyuo vingine wakafanye bidii ili vyuo hivyo viweze kuendelea na kuvutiwa na wahitimu hao kutoka TIA na kwa wale watakaobahatika kufanya kazi basi wakafanye kazi kwa umahiri na maadili ili kuendeleza taswira nzuri ya TIA.
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia kwenye mahafali hayo.
Wahadhiri wa TIA Kampasi ya Singida wakiwa kwenye mahafali hayo.
Wahitimu wakitunukiwa vyeti vyao kwenye mahafali hayo.
0 Comments