Naibu
Meya Manispaa ya Kinondon,Songoro Mnyonge (katikati), akiongea na waandishi wa
habari Agosti 12, 2014 jijini Dar es Salaam mara bara baada
ya kufungua kikao kilichowakutanisha wakuu wa shule, watendaji wa mitaa, kata
pamoja na wenyeviti wa bodi za shule chenye lengo la kuangali namna ya
kupatikana kwa fedha za kujenga zinajenga maabara katika shule za
Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu (kushoto), Afisa Uhusiano Manispaa ya
Kinondoni, Sebastian Mhowera, na kulia. Diwani Kata ya Kawe Othmani Chipeta.
HABARI PICHA. NA
PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWEBLOG
+255787942222
.............................
MANISPAA
ya Kinondoni inahitaji jumla ya kiasi cha Sh Bilioni 1.3 ili kutekeleza
agizo la Rais Jakaya Kikwete aliyezitaka Halmashauri zote kuhakikisha zinajenga
maabara katika shule za Sekondari ifikapo Novemba Mwaka huu.
Hayo
yamebainishwa jana Jijini Dar es salaam na Naibu Meya wa Manispaa hiyo Songoro
Mnyonge wakati akizungumza katika kikao kilichowakutanisha wadau
mbalimbali wakiwemo wakuu wa shule, watendaji wa mitaa, kata pamoja na
wenyeviti wa bodi za shule chenye lengo la kuangali namna ya kupatikana kwa
fedha hizo.
Huku
akiwaomba wadau mbalimbali yakiwemo mashirika, taasisi, watu binafsi pamoja na
wafanyabiashara kujitokeza kuchangia upatikanaji wa fedha hizo, Songoro alisema
ushirikiano wao katika suala hilo utaipa faraja manispaa hiyo kutokana na
umuhimu wa elimu kwa taifa.
“Tunawaomba
mjitokeze kwa wingi ili kuunga mkono juhudi za Rais Kikwete anayetaka kuona
shule zote za sekondari zinakuwa na maabara za kudumu ili kusaidia kupanua wigo
wa ufundishaji kw wanafunzi mashuleni, jitihada zetu pekee hazitotuwezesha
kufikia malengo hayo kutokana na ufinyu wa bajeti” alisema Mnyonge.
Aidha
alisema manispaa hiyo inahitaji maabara za kudumu 114 kukidhi mahitaji katika kata
32 huku sekondari 14 ndizo pekee katika zilizo na maabara hizo kati ya 46
zilizopo katika manispaa hiyo suala alilosema linahitaji kutafutiwa ufumbuzi wa
haraka.
Alisema
kila chumba kimoja cha maabara ya kudumu ujenzi wake unakadiriwa kufikia kiasi
cha Sh Milioni 75 na kwa jumla ya vyumba vote 114 inahitajika kiasi hicho cha
zaidi ya Sh Billioni 1,suala alilosema haliwezi kufanikiwa bila nguvu za wadau
mbalimbali.
Alisema
malengo ya baadae ya manispaa hiyo ni kujenga vyumba vitatu vya maabara ya
fikizia, kemia na baiolojia ifikapo mwaka 2016 hatu aliyosema kwa kiasi kikubwa
itamaliza tatizo la ugumu wa masomo ya sayansi kwa wanafunzi sambamba na
kuongeza wataalam wa baadae wa Taifa hili.
|