Mfaransa Yohann Diniz, aliyeshiriki kwenye mashindano ya
mbio za kutembea za kilometa 50, amesitaajabisha ulimwengu le baada ya kamera
ya video kumpiga picha akiwa anajisadia haja kubwa kwenye kaptura yake wakati
wa mashindano huko Rio kwenye Olimpiki.
Awali kabla ya mashindano kuanza, Mfaransa huyo alilamika
kusumbuliwa na tumbo, lakini akaendelea kushiriki mashindano ambapo baada ya
muda alianguka nchini na mmoja katika ya washiriki wenzie akamsadia kumnyanyua
na wakaendelea na mashindano kabla ya tumbo kumzidia na kuamua kujisadia
katikati ya mashindano hayo.
Kabla ya hayo, Yohann Diniz alikuwa akiongoza mbio hizo
lakini aliishia kupata nafasi ya 11,licha ya maswahiba hayo yaliyomkuta ya
kuanguka njiani na kujisaidia katikati ya mashindano.




